Social Icons

Pages

Featured Posts

Tuesday, December 08, 2015

RC MWANZA ASIMAMISHA VIGOGO WATATU


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo, amewasimamisha kazi watumshi watatu wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema, kutokana na kuruhusu ujenzi wa nyumba juu la bomba la mradi wa maji na kuamuru ivunjwe mara moja.

DK. SHEIN SASA AWASHUKIA WATAALAM WA AFYA Z'BAR


Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein.
Wahitimu wa Chuo cha Taaluma za Sayansi za Afya Zanzibar, wametakiwa kuacha tabia ya kupiga chenga wanapopangiwa kufanya kazi kisiwani Pemba jambo linalosababisha upungufu wa wataalam katika sekta ya afya kisiwani hapa.

MENEJA MKUU KIWANDA CHA URAFIKI ASIMAMISHWA KAZI

Kiwanda cha Nguo cha Urafiki.
Serikali kupitia Wizara ya Viwanda na Biashara, imeingilia kati mgogoro wa Kiwanda cha Nguo cha Urafiki kwa kuwasimamisha kazi Meneja Mkuu wa kiwanda hicho, Nassoro Baraza na Naibu Meneja Mkuu, Samweli Swai ili kupisha uchunguzi dhidi yao ufanyike na endapo watabainika kuwa ni chanzo cha mgogoro huo watachukuliwa hatua za kisheria.

WAILALAMIKIA DAWASCO KUKOSA MAJI MIEZI MITATU


Wananchi  na wamiliki wa viwanda katika eneo la Salasala Kinondoni, jijini Dar es Salaam, wamelilalamikia Shirika la Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (Dawasco), kwa kushindwa kuwapa huduma ya maji kwa takribani miezi mitatu sasa.

MNYIKA ATAKA RIPOTI ZA MWAKYEMBE, SITTA KUHUSU BANDARI

Mbunge wa Jimbo la Kibamba, John Mnyika, ameomba ripoti za kamati za uchunguzi zilizoundwa na mawaziri wa Wizara ya Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe na Samuel Sitta, kuhusu Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) ziwekwe hadharani.