Social Icons

Pages

Tuesday, May 26, 2015

RESOLUTION YAFANYA MASHINDANO YA KUJIJENGA - JANGWANI SEA BREEZE

Picha ya pamoja ya wafanyakazi wa Bima ya Resolution Dar es Salaam, walishiriki mashindano ya kujijenga kikazi zaidi, ambapo walicheza michezo mbalimbali na Timu Kibo iliibuka kwa ushindi wa jumla na kuondoka na Medali za Dhahabu, huku Timu Mawenzi wakiambulia Medali za Fedha.

Timu Mawenzi ikijiandaa na mashindano ya mpira wa ufukweni, Deuce "Kaghasheki" akitoa maelekezo kwa timu yake, jinsi ya kuwashinda wapinzani wao Timu ya Kibo
Nayo Timu Kibo ikijipanga kuwakabili wapinzani wao, hii ni picha ya pamoja kuonesha mshikamano wa kuwadhibiti timu pinzani
Wachezaji wa kipindi cha kwanza Timu Kibo Wanaume kutoka kushoto Alphonce 'Kiungo Mkabaji', Gerrard 'Kiungo wa Kati' Oscar 'Kocha Mchezaji', Mrisho 'Kiungo Mchezeshaji' na Ismail 'Mlinda Mlango' wakiwa tayari kwa mpambano.
Penati iliowaondoa Timu Kibo Wanaume, inakwenda kupigwa na mshambuliaji hatari wa Timu Mawenzi Emmanuel (wa kwanza kushoto), huku Captain wa Hawamu akitoka nje baada ya maumivu aliochezewa rafu mbaya. Mawezi 2 - 1 Kibo.
Mshambuliaji hatari wa Timu Kibo Zamaradi akipangua ngome ya Mawenzi, na kuachia shuti kali lililomzidi mlinda lango wa Mawezi Janet na kuibuka na ushindi wa goli moja dhidi yao. Hadi mwisho wa mchezo huo Kibo Wanawake 1 - 0 Mawenzi Wanawake.
Timu ya Madaktari George Ngongi (kushoto) na Mama Batuly wakiendelea na kutoa huduma mbalimbali kwa wateja wa Bima ya Resolution. Resolution kazi popote, mteja hapotei hapa. Big up Madokta wetu.
Timu Kibo wakijianda kuvuta kamba
Timu Mawenzi nao wapo tayari kuwaonesha uwezo wapinzani. Pambano hili halikuwa na mshindi...
Wahamasishaji wa Timu Kibo Harrieth na Zulfa.
Wazee wa Mipango Mkakati Auson na Thadei, wakitafakari michezo wa awali.
Mtaalamu mpira wa mezani "pool table" Timu Kibo Andy akimtoa jasho mpinzani wake wa Timu Mawenzi Kaaya (hayupo pichani).
Timu Kibo wakijiandaa kucheza mpira wa mtipio (rede). Kepteni Andy akitoa mbinu kwa Zamaradi jinsi ya kuushinda mchezo.
Timu Mawenzi walitoa ushindani mkubwa katika mchezo. Keptain Eunice (mwenye pedo nyeupe) aliibuka mchezaji bora katika mchezo wa rede.
Timu Kibo wakifurahia mchezo wa rede.
Maina wa Timu Mawenzi aliefungwa kitambaa, akiongozwa na Haika kutembea na kikombe kilichojaa maji kutembea nacho mita 50 bila kumwagika chini.
Timu  Mawenzi wakionekana kuwania mpira kutoa kwa wapinzani wao Timu Kibo. Mchezo wa Nyavu (Volleyball) ndio ulikuwa fainali ya michezo yote ya siku hio.
Oscar 'Kocha Mchezaji' akifurahia ushindi wa Timu Kibo kwa kula medali. Hii haijawai tokea...
Kepteni wa Timu Mawenzi Hawamu Didier, na Keptini wa Timu Kibo Andy Seka wakionesha medali zao kwa pamoja.
Washindi wa pili Timu Mawenzi wakifurahia kwa kuonesha Medali zao za Fedha.
Mabingwa Timu Kibo wakionesha Medali zao za Dhahabu kwa fuhara zaidi. Hii ni zaidi ya stori..........

No comments: