Pazia la Chama cha
Mapinduzi (CCM) kupata mgombea wake wa urais katika Uchaguzi Mkuu wa
Oktoba limefunguliwa rasmi jana mjini Dodoma.
Makada wanne walichukua fomu za kuwania nafasi
hiyo, huku wakisindikizwa na wapambe wao na kukutana na Katibu wa
Oganaizesheni, Dk Mohamed Seif Khatib aliyewakabidhi fomu hizo, katika
ofisi za makao makuu ya chama hicho.
Shughuli hiyo ilitawaliwa na kila aina ya
mbwembwe, shangwe na shamrashamra, hasa wakati wagombea hao walipokuwa
wakizungumza na waandishi wa habari na kueleza mikakati yao ya kwenda
Ikulu.
Waliochukua fomu jana ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais (Kazi Maalumu), Profesa Mark Mwandosya, Waziri wa Kilimo, Chakula
na Ushirika, Stephen Wasira, Balozi wa Kudumu wa Umoja wa Afrika (AU),
katika Umoja wa Mataifa (UN), Amina Salum na Mbunge wa Afrika Mashariki,
Makongoro Nyerere.
Wakati makada hao wakitangulia, leo ni zamu ya
wengine wakiwamo Makamu wa Rais Dk Mohamed Gharib Bilal na Waziri wa
Ujenzi, Dk John Magufuli, ambao tofauti na makada wengine, hawakuitisha
mikutano ya kutangaza nia.
Kwa mujibu wa ratiba ya jana, mmoja kati ya
waliotarajiwa kuchukua fomu alikuwa Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa
lakini alishindwa ikielezwa kuwa alikuwa katika msiba wa Mbunge wa
Ukonga, Eugen Mwaiposa.
Mbwembwe
Wagombea waliokuwa kivutio tangu katika uchukuaji
wa fomu hadi kujibu maswali ya wanahabari ni Makongoro na Wasira, huku
Profesa Mwandosya akiwaponda wagombea urais wanaojikita kuwaponda
wenzao, badala ya kueleza watalifanyia nini Taifa. Mgombea wa kwanza
kufika katika ofisi hizo akiwa na msafara wa magari manne na wapambe
takriban 100 alikuwa Profesa Mwan dosya. Aliambatana na wabunge, Profesa
David Mwakyusa (Rungwe Magharibi), Abdul Marombwa (Kibiti), Aliko
Kibona (Ileje), Hilda Ngoye (Viti maalumu) na Mchungaji Lackson Mwanjali
(Mbeya Vijijini).
Baadaye alifuatia Wasira, kisha Amina ambaye
aliambatana na Mbunge wa Viti maalumu, Anna Abdallah huku Makongoro
akifunga pazia la uchukuaji huo wa fomu jana.
Wasira na Profesa Mwandosya waliambatana na wake zao, huku Makongoro na Amina wakiwa na wapambe tu.
Dk Bilal na Dk Magufuli
Uchukuaji wa fomu unaendelea tena leo kuanzia saa
nne asubuhi hadi saa 12 jioni na miongoni wanaotarajiwa ni Dk Bilal, Dk
Magufuli, Amos Siyatenzi, Waziri Mkuu mstaafu Frederick Sumaye, Balozi
Ali Karume na Lowassa.
Profesa Mwandosya
Wasira
Ali Karume na Lowassa.
WanaCCM ambao wametangaza nia ya kugombea urais ni Waziri wa
Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, Profesa Sospeter Muhongo, Naibu
Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia, January Makamba, Naibu
Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba, Mbunge wa Kisesa Luhaga Mpina, Waziri
wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk Titus Kamani, Waziri Mkuu Mizengo
Pinda na Mbunge wa Nzega Dk Hamis Kigwangalla.
Profesa Mwandosya
Alitumia dakika 53 katika mkutano wake na
waandishi wa habari baada ya kuchukua fomu, kueleza masuala mbalimbali
atakayoyafanya iwapo atakuwa rais. Mbali ya kukerwa na wanaowaponda
wenzao akiwataka kueleza watalifanyia nini Taifa, alisema: “Kuchukua
fomu leo (jana) ni hatua ya kuelekea katika jumba jeupe (Ikulu). Uamuzi
huu ni mzito lakini nimejiandaa kiakili, kiafya na kimaono.”
Mwandosya ambaye alijitosa kuwania urais mwaka
2005 na kushika nafasi ya tatu, nyuma ya Dk Salim Ahmed Salim na Rais
Jakaya Kikwete alisema, “Wagombea wamejitokeza wengi sana. Mimi hii ni
mara yangu ya pili na wingi huu unaonyesha ukomavu wa demokrasia.”
Aliposhika nafasi ya tatu 2005, alivishwa taji la
shaba, kwamba safari hii atavikwa taji la dhahabu kwa sababu hafikirii
kushindwa na kwamba CCM kitampima kwa rekodi yake.
“Sababu kubwa si urais wala mambo yanayofuatana na
urais kama kupigiwa ving’ora, misururu ya magari na kupigiwa saluti.
Kubwa zaidi ni kukijenga chama. Rais bora atatoka CCM na nitaendelea
pale alipoishia Rais Kikwete, nitaondoa umaskini na kuifanya Tanzania
kuwa nchi iliyoendelea kwa kujenga misingi imara,” alisema.
Akijibu swali juu ya uzoefu wake na alivyoshindwa
kupenya mwaka 2005 alisema: “Imepita miaka 10 tangu niwanie urais, sasa
nina uzoefu wa kutosha serikalini ni tofauti na mtu anayetokea nje ya
mfumo wa Serikali.”
Akizungumzia ukosefu wa ajira kwa vijana alisema
jambo hilo litamalizwa kwa kuwawezesha vijana kujiajiri ili nao waweze
kuwaajiri vijana wenzao.
Wasira
Wasira alisema katika kipindi alichotumikia
Serikali katika ngazi tofauti ameandaliwa vizuri: “Uchumi wa kisasa
ambao haujali maisha ya watu hauna maana.”
Wasira alipoulizwa atawezaje kutekeleza sera ya
chama chake ya ujamaa na kujitegemea katika kuifanya nchi kukua kiuchumi
alisema, China ni wanachama wa ukomunisti lakini ni miongoni mwa nchi
ambazo uchumi wake unakuwa kwa kasi kubwa... “Ubepari ni mfumo wa
mashindano ambao wananchi maskini hawawezi kuondoka katika umaskini
lakini ujamaa unajali maisha ya watu wote.”
Alisema kila wakati nchi inakuwa na vipaumbele
vyake na kwamba katika kipindi alichokuwapo serikalini wameweza
kuanzisha benki ya kilimo. “Siyo kwamba tupo kama tulivyokuwa. Umaskini uliokuwapo mwaka
1961 siyo kama uliopo sasa, tumeendelea kupambana nao,” alisema Wasira.
Amina
Makongoro
Hata hivyo, alisema bado hawajawekeza vizuri
katika kilimo kwa kutilia mkazo kwenye utafiti, umwagiliaji, ugani na
mkopo. Kuhusu kukaa muda mrefu serikalini, alisema hiyo hoja, bali mtu
amefanya nini?.. “Rais anatakiwa awe na upeo, anayejua historia na kujua
mahitaji ya sasa na siku zijazo, hoja si kukaa muda mrefu.”
Alipoulizwa haoni kama historia yake ya kutoka
ndani ya chama na kurejea inaweza kumkwamisha, Wassira alisema chama
kina misingi, kanuni na taratibu zake: “Hakuna mahali panapoeleza kuwa
ukitoka ndani ya chama na kurudi unapewa hukumu ya kifo.”
Kuhusu kauli aliyowahi kuitoa ya kuwa yeye si mvua
nchi ilipokumbwa na tatizo la njaa, Wasira aliwataka Watanzania
kumwamini kuwa atahimili nafasi ya urais endapo atafanikiwa kuipata.
Amina
Amina ambaye amewahi kuwa waziri alisema
ataipeleka Tanzania katika uchumi wa kati na mpango huo utakwenda
sambamba na kumaliza kabisa rushwa na ufisadi na kuinua sekta ya
viwanda.
Alijikita katika ajenda tatu; uchumi, kupunguza
umaskini na kuboresha zaidi huduma za jamii. Alisema ili nchi iweze
kupiga hatua, ni lazima kuwepo na viwanda vitakavyowezesha kukua kwa
sekta ya kilimo.
“Lazima tubadili aina ya ufanyaji kazi ili tuweze
kupata maendeleo. Lazima tuboreshe miundombinu ya reli, barabara na
anga. Nchi yetu imekuwa na pengo la wenye nacho na wasionacho na katika
kumaliza hili ni lazima tuunganishe elimu na ajira,” alisema.
Kuhusu rushwa alisema lazima iwepo Mahakama
maalumu ya kushughulikia kesi za rushwa huku akizungumzia kubana
matumizi kwa kuwa na vyanzo vya ndani vya mapato, kuacha kutegemea
wafanyabiashara na nchi wahisani.
Makongoro
Makongoro alisema baadhi ya wanachama wa CCM
wanapohusika na rushwa na kisha kuhojiwa na vyombo vya dola vilivyowekwa
kisheria, wamekuwa wakitoa majibu yasiyoridhisha.
“Kama watu wamekula rushwa na wanatumia nafasi
hiyo kama dhamana waliyopewa katika chama kinachosema cheo ni dhamana.
Halafu idadi ya watu kama hao inaongezeka kama uyoga hiyo inafanya imani
ya watu katika chama iwe ndogo,” alisema.
Alisema ni bahati mbaya kwamba ndani ya CCM kuna makundi ambayo
si ya itikadi bali ya uhasama... “Kimsingi makundi haya yanatokana na
kuwapo kwa mmoja wao aliyemzidi mwenzie katika kuchota fedha zetu
hazina,” alisema.
Alisema hata Rais Jakaya Kikwete anapowaambia
wanaCCM waachane na makundi ya uhasama, wasitoe rushwa wala kukiuka
utaratibu wamekuwa hawafuati kwa sababu ya usugu. Alisema kuwa
atarudisha fomu zake mjini Dodoma Juni 20.
CHANZO: MW3ANANCHI
CHANZO: MW3ANANCHI

No comments:
Post a Comment