Waziri wa Fedha, Saada Mkuya.
Serikali imesema kuwa inafanya utaratibu wa
kuwalipa fedha takribani Sh. bilioni 19 za waliokuwa wanachama wa
Taasisi ya Development Entrepreneurship Community Initiative (DECI).Akizungumza na NIPASHE kwa njia ya simu, Waziri wa Fedha, Saada
Mkuya, alisema fedha hizo zimehifadhiwa katika akaunti ya Benki Kuu
(BoT) na kwamba kinachofanyika sasa ni uangalizi wa kiasi cha michango
iliyochangwa na wanachama ili waweze kulipwa kwa usahihi.
“Bado fedha zinashikiliwa BoT uchambuzi unaendelea kufanywa kwa
umakini wa hali ya juu, utakapokamilika wanachama wote waliochanga fedha
watalipwa,” alisema Mkuya. Aidha, Waziri Mkuya alisema siyo jambo litakaloweza kuchukua muda
mfupi kukamilisha mchakato wa malipo ya wanachama hao, kwani linahitaji
muda wa kutosha kufanyiwa kazi kikamilifu, ingawa hakutaja kiasi
kilichopo.
Mwaka 2009 serikali ilisitisha shughuli za Deci na kuwafungulia
mashtaka wakurugenzi watano wa taasisi hiyo katika Mahakama ya Hakimu
Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam na Agosti 19, mwaka 2013,
walihukumiwa.
CHANZO:
NIPASHE

No comments:
Post a Comment