
Mbunge wa Viti Maaalum Chadema, Suzan Lyimo.
Wabunge wamefichua ufisadi katika Hospitali ya Rufaa
ya KCMC, mkoani Kilimanjaro, ambayo watendaji wakuu wa hospitali hiyo
wameuziana magari mapya ya serikali kwa bei ya kutupa ya Sh. milioni 8
kila moja.
Ubadhirifu huo ni wa kutisha uliibuliwa jana Bungeni wakati mjadala
wa hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa mwaka wa
fedha wa 2015/2016. Mbunge wa Viti Maaalum Chadema, Suzan Lyimo, alisema viongozi wakuu
KCMC wameuziana magari aina ya Prado na Nissani Patro kwa bei ya Sh.
milioni 8 kila moja mwaka 2013, ambayo yalipelekwa katika hospitali hiyo
kwa shughuli mbalimbali.
Alisema kutokana na ubadhirifu huo Mhasibu wa hospitali hiyo, Paulo
Muhunya, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Afya
(TUGHE), alimjulisha Rais Jakaya Kikwete, kwa kumtumia ujumbe mfupi wa
maneno (SMS) kuhusu ufisadi huo. Lyimo alisema katika hali ya kushangaza Mhasibu huyo baada ya kutoa
taarifa za ubadhirifu huo, Mei 5, mwaka huu, alisimamishwa kazi jambo
ambalo linatia mashaka.
"Nchi hii inashangaza inakuweje mtu aliyesaidia kutoa taarifa za
kufichua wizi yeye ndiye anaadhibiwa, au ndio utaratibu wa serikali ya
CCM kuwalinda wezi," alisema. Naye Mbunge wa Viti Maalum Chadema, Congesta Lwamlaza, alisema
Serikali ya CCM ni ya kutumbua tu ndiyo maana fedha nyingi zinatengwa
kwa mambo ya starehe tu.
CHANZO:
NIPASHE

No comments:
Post a Comment