Mkurugenzi wa AFB, Karl Westvig.
Kampuni ya Huduma za Kifedha ya AFB inayojihusisha
na kutoa ushauri na huduma za kifedha kwa wajasiriamali, imeingia
mkataba wa Dola milioni 20 na kampuni ya Gemcorp inayojihusisha na
uwekezaji wenye mtazamo wa masuala ya kimasoko.Akizungumzia mkataba huo, Mkurugenzi wa AFB, Karl Westvig, alisema:
“Nimefarijika sana kuingia makataba huu ambao umekuja kwa wakati
mwafaka ambao pia ni muhimu sana kwa kampuni. Uwekezaji huu wenye
mantiki kutoka kwa Gemcorp utatoa mchango mkubwa sana katika kuleta
maendeleo Kusini mwa Jangwa la Sahara.”
Kwa sasa AFB ipo pia katika mataifa ya Ghana, Kenya, Zambia na
Tanzania, huku ikiwa na mpango wa kujitanua katika nchi nyingine za
Afrika ifikapo mwaka 2020 ikiwa na bidhaa zenye ubunifu na ufumbuzi na
zenye kukidhi vigezo vyote sokoni.
Kwa mujibu wa ripoti ya Benki ya Dunia, zaidi ya watu milioni 400
waliopo Kusini mwa Jangwa la Sahara bado wanafanya shughuli zao nje ya
mfumo rasmi wa kifedha.
Akizungumzia juu ya uwekezaji huo, Mkurugenzi wa Gemcorp, Atanas Bostandjiev, alisema: “Huduma za kifedha ni sekta muhimu kwa mustakabali wa kampuni yetu
na tumekuwa tukiangalia hasa soko la Afrika, AFB ni fursa kubwa ya
kiuwekezaji kwetu. Ikiwa na lengo la kutekeleza maendeleo ya kifedha
kupitia ufumbuzi wa kiteknolojia, kampuni hii inalenga kuharakisha
ukuaji wa maendeleo kulingana na mahitaji ya Bara la Afrika hasa kwa
tabaka la kati.”
Alisema anaamini kwamba wataendelea kufanya kazi kwa pamoja na kuendeleza ushirikiano kwa maendeleo ya AFB.
CHANZO:
NIPASHE

No comments:
Post a Comment