Social Icons

Pages

Thursday, June 04, 2015

RC AZIPA CHANGAMOTO KAMPUNI ZA SIMU NCHINI

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas T. Gama aikata utepe kuzindua rasmi Tawi la Tigo Moshi Mjini jana, wanaoshuhudia kulia ni Gwamaka Mwakilembe, Meneja huduma kwa wateja Kanda ya Kaskazini.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama, amezishauri kampuni za simu za mkononi kuhakikisha inawekeza katika mtandao wa elimu ili kuwarahisishia wanafunzi wa vyuo katika sekta ya elimu na kuboresha huduma zake kwa wateja.
Gama alitoa rai hiyo alipozindua Duka jipya la Tigo mjini Moshi jana. Alisema ili kuhakikisha kuwa kampuni hiyo inakua kila uchao, ni lazima kuhakikisha kuwa wanazidi kuboresha huduma zake kwa wateja ikiwamo kuwekeza katika sekta ya elimu.
Alisema katika kuhakikisha elimu inakua kwa kasi na kufanya ushindani mkubwa katika soko la ajira za Afrika Mashariki, kampuni za simu zihakikishe zinatoa  fursa kwa wanafunzi kupata masuala mengi zaidi kwa ajili ya kuleta mabadiliko.
“Tigo ni moja ya kampuni za simu ambazo zimekuwa zikikua kwa kasi kubwa hapa nchini na kusababisha ushindani mkubwa na mitandao mingine. Sasa imefika wakati kampuni hii kuangalia upya uwezekano wa kuwekeza katika sekta ya elimu ili kuwanufaisha wanafunzi na wanavyuo wote katika kuhakikisha kuwa wanapata kiurahisi huduma ya kielimu,” alisema Gama.
Awali, akisoma risala kwa Mkuu wa Mkoa, Meneja wa Ubora wa Huduma kwa Wateja wa Tigo, Mwangaza Matotola, alisema duka hilo jipya limefunguliwa kwa lengo la kuhakikisha kuwa linawaondolea usumbufu wateja wa mtandao huo ambao walikuwa wakisubiri huduma kwa muda mrefu katika duka moja la mjini Moshi.
Matotola alisema uzinduzi wa duka hilo umefanyika ikiwa ni siku moja baada ya kampuni hiyo kufungua duka lingine lililokarabatiwa jijini Arusha, lengo likiwa ni kuboresha na kusogeza huduma karibu zaidi na wateja wake.
CHANZO: NIPASHE

No comments: