Social Icons

Pages

Thursday, June 04, 2015

BILAL, LOWASSA, MAGUFULI KUPIGANA VIKUMBO LEO


Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal.
Mji wa Dodoma na viunga vyake, leo unatarajiwa kuwaka moto baada ya vigogo sita wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) watakapokuwa wanachukua fomu ya kuwania urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Vigogo wanaochukua fomu leo ni pamoja na Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal, Mawaziri Wakuu wastaafu, Edward Lowassa na Frederick Sumaye, Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta na Balozi Ali Abeid Karume.
Mbali ya vigogo hao sita, pia yupo kada mwingine wa chama hicho, Amosi Siyatemi, anayelezwa kuwa ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu Mzumbe. Idadi hiyo ya wanaochukua fomu za kuomba kuwania urais itafikisha jumla ya makada 11 wa CCM ambao tayari wamekwisha kuchukua fomu za kuomba ridhaa kwa chama chao kuwania nafasi ya juu ya uongozi nchini.
Wengine waliochukua fomu jana ni Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Steven Wasira, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Kazi Maalum), Prof. Mark Mwandosya, Mbunge wa Afrika Mashariki, Makongoro Nyerere na Balozi Amina Salum Ali.
Lowassa alitakiwa kuchukua fomu jana, lakini aliahirisha kutokana na msiba wa Mbunge wa Ukonga, marehemu  Eugen Mwaiposa, aliyefariki dunia usiku wa kuamkia juzi mjini Dodoma.
Kwa mujibu wa ratiba hiyo, wa kwanza kuchukua fomu atakuwa Siyatemi, akifuatiwa na Sumaye, Dk. Bilal, Balozi Karume, Lowassa na atakayefunga dimba ni Dk. Magufuli.
CHANZO: NIPASHE

No comments: