Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Issa Machibya, ameagiza
kusakwa kwa wanafunzi 3,076 ambao hawajajiunga na kidato cha kwanza
katika shule za sekondari za serikali mkoani hapa mwaka huu.Machibya alitoa agizo hilo jana wakati akizungumza na waandishi wa
habari kuhusiana na wanafunzi hao ambao ni kati ya waliochaguliwa
kujiunga na kidato cha kwanza baada ya kufaulu mtihani wa taifa wa
darasa la saba mwaka jana.
Alisema ametoa agizo hilo kwa maofisa elimu wa shule za sekondari,
bodi za shule kushirikiana na kamati za maendeleo za kata mkoani hapa
kuhakikisha wanawasaka wanafunzi hao, kuwakamata wazazi wao na
kuwafikisha mahakamani kwa kushindwa kuwapeka shule.3
Kwa mujibu wa Machibya, Wilaya ya Uvinza inaongoza kuwa na idadi
kubwa ya wanafunzi wasioripoti shuleni 732 ambao ni sawa na asilimia
39.48 ya wanafunzi 1,854 waliochaguliwa katika Wilaya hiyo. “Iasikitisha sana watoto wetu ambao tunaishi nao nyumbani
mmeshindwa kuwapeleka shuleni kinyume cha sera ya elimu inayomtaka kila
mwanafunzi aliyechaguliwa kuripoti shuleni na kuanza masomo hadi
kumaliza kidato cha nne, " alisema na kusisitiza kuwa: " Wazazi wote
ambao watoto wao waliochaguliwa hawajaripoti shule wahakikishe
wanawapeleka shuleni kabla ya Machi 30 mwaka huu vinginevyo watakamatwa
na kufikishwa mahakamani."
Aliwataka wakuu wa sekondari kutoa ushirikiano kwa wazazi kwa
kuwapokea wanafunzi waliochaguliwa hata kama hawana sare ya shule, ada
na michango.
CHANZO:
NIPASHE
No comments:
Post a Comment