
Mwanafunzi Juma Hussein akitoa maelekezo ya jinsi mfumo wa damu
unavyofanya kazi mbele ya Rais Jakaya Kikwete hivi karibuni.
Ni mtoto wa kwanza kati ya watoto watatu wa Mzee Hussein aliyepanga eneo la Kipunguni, Ilala jijini Dar es Salaam. Hasiti kusema kuwa familia yake inaishi katika
maisha duni. Kwa mfano, anasema ili maisha yaende mama yake ameamua
kuuza pombe za kienyeji eneo la Gongolamboto, huku baba yake wa kambo
akiwa ni dereva wa moja ya magari yanayosambaza bidhaa za kampuni ya
Said Salim Bakhresa.
Ni mfano wa watoto waliozoea hali ya ugumu wa
maisha, kwani kipato kinachoendesha familia yao ni kidogo hali
inayomfanya asome katika mazingira magumu. Kila siku asubuhi hukabidhiwa
Sh1,200 tu kwa usafiri wa mabasi ya daladala na pia chakula awapo
shuleni.
Anaitwa Juma Hussein, mwanafunzi wa kidato cha nne
katika shule ya Sekondari ya Majani ya Chai, ambaye mara kadhaa
huonekana kwa sura ya unyonge licha ya kuwa ni miongoni mwa wanafunzi
wanaoongoza kwa ufaulu darasani. Mwananchi ilimwomba kuzungumza naye baada ya
kuonyesha uwezo mkubwa wa kuelezea mfumo wa damu unavyofanya kazi
mwilini mbele ya Rais Jakaya Kikwete.
Tukio hilo lilifanyika siku kadhaa zilizopita
ikiwa ni sehemu ya uzinduzi wa sera mpya ya elimu nchini. Shule hiyo
ilichaguliwa na Rais kwa kigezo cha kutimiza ahadi ya ujenzi wa maabara
zote katika muda uliopangwa.
Uso kwa uso na Rais Kikwete
Kwa lugha ya mazingira ya kishule, Juma anaweza
kuambiwa kuwa siku hiyo alijizolea ‘ujiko yaani sifa. Hii siyo kwa
kukutana na kiongozi wa nchi, lakini pia kwa kumvutia kutokana na
maelezo fasaha aliyokuwa akimweleza kuhusu mada ya mfumo wa damu
unavyofanya kazi mwilini.
Kwa hakika alimshangaza Rais na watu waliombatana
naye siku hiyo, huku yeye mwenyewe akisema ujasiri wa kuzungumza mbele
ya Rais na wageni wengine maarufu kwa mara ya kwanza ulitokana na
kujiamini.
“Nilimwona Rais Kikwete kama mtu wa kawaida kama
wengine waliokuwa kwenye tukio lile. Hali hiyo ilinisaidia kufanya
vizuri, kwani kama ningemchukulia kama kiongozi wa nchi labda ningeogopa
na kufanya vibaya, lakini nashukuru kazi ilifanyika vizuri tu.”
Akiwa na sura ya kinyonge na hulka ya kuzungumza
taratibu, Juma anasikitika kuwa fursa aliyopata ya kukutana uso kwa uso
na Rais Kikwete, hakuitumia kumweleza mambo matatu anayoamini ni muhimu
hasa katika fani za uhandisi na Tehama. Ni mambo gani hayo?
Anasema: “Ningemwomba ahakikishe anaondoka
madarakani akiwa ameacha shule zote za sekondari zikiwa na maabara za
masomo ya sayansi, walimu wa kutosha na kuondoa vikwazo vinavyowakabili
wanafunzi wenye ndoto za kusoma sayansi,’’
Mchango wa familia yake
CHANZO: MWANANCHI
Siri za mwanafunzi kufanya vyema
Juma anasema zipo njia mbili tu zinazoweza
kumsaidia mwanafunzi yeyote yule nchini kufanikiwa katika ndoto zake za
kufanya vizuri katika masomo ya sayansi. Njia hizo anataja kuwa ni juhudi binafsi na mchango wa mazingira yanayomzunguka mwanafunzi.
“Kwanza ni kuamua kupenda somo lenyewe, hali ya kupenda inajengwa na hisia za mwanafunzi mwenyewe, hivyo unaweza kuhamishia hisia zako kwenye masomo hayo. Ukifanya hivyo itakuwa hatua ya kwanza na muhimu sana,” anasema na kuongeza: “Najua mwanafunzi anaweza kuathiriwa na ugumu wa maisha nyumbani, lakini hali hiyo lazima aichukulie kama changamoto na pia iwe kama hasira kwake ya kujituma zaidi, kujisomea na kuwekeza nguvu na muda mwingi akifikiria masomo. Mimi kama ningefikiria sana changamoto za familia yangu nisingeweza kuwa na juhudi hizi.”
“Kwanza ni kuamua kupenda somo lenyewe, hali ya kupenda inajengwa na hisia za mwanafunzi mwenyewe, hivyo unaweza kuhamishia hisia zako kwenye masomo hayo. Ukifanya hivyo itakuwa hatua ya kwanza na muhimu sana,” anasema na kuongeza: “Najua mwanafunzi anaweza kuathiriwa na ugumu wa maisha nyumbani, lakini hali hiyo lazima aichukulie kama changamoto na pia iwe kama hasira kwake ya kujituma zaidi, kujisomea na kuwekeza nguvu na muda mwingi akifikiria masomo. Mimi kama ningefikiria sana changamoto za familia yangu nisingeweza kuwa na juhudi hizi.”
Kuhusu sababu ya pili ambayo ni mazingira
yanayomzunguka mwanafunzi, anatolea mfano wa masomo ya sayansi ambayo
wanafunzi hawawezi kufanya vizuri kama hakuna mazingira bora kama vile
miundombinu ya maabara na ushiriki wa wazazi katika kuhamasisha watoto.
Anaongeza: “Kuna mchango mkubwa unaohitajika
kutoka serikalini kuhakikisha inaandaa walimu wa kutosha katika masomo
ya sayansi nchini nzima na kuweka maabara za kutosha.” Anasema mwanafunzi anaweza kuwa na dhamira, nia ya kusoma lakini kama hakuna miundombinu mizuri ndoto zinaweza kupotea.
Wosia kwa wanafunzi
Kwa upande mwingine, Juma anasema jitihada za
ujenzi wa miundombinu shuleni na uwekezaji wowote wa elimu unaofanywa na
Serikali, vinaweza kukosa tija ikiwa wanafunzi hawana ari ya kujifunza. “Huwezi kupenda sayansi halafu ukachagua rafiki
anayependa michezo tu shuleni au unakuwa na rafiki asiyezingatia masomo
na tabia zake ni chafu, haifai kabisa,” anaeleza.
Mchango wa familia yake
Juma anasema japo familia yao ni ya kipato cha kawaida, baba
yake mlezi, aliahidi kumsaidia kielimu ili atimize ndoto yake ya kufika
chuo kikuu. Anashukuru kuwa familia yake imeamua kumpa msaada wa
kutimiza ndoto zake. “Najua mama hawezi lakini baba aliniambia
atanisaidia kwa nafasi yake mpaka nitakapofanikisha ndoto zangu. Ndoto
zangu ni kusoma masomo ya Fizikia, Kemia na Bailojia ili baadaye nije
kuvaa kofia ya udaktari, kwa sababu ninaliweza kwa kiwango kikubwa somo
la Baiolojia.
CHANZO: MWANANCHI
No comments:
Post a Comment