Rais Jakaya Kikwete amesema baadhi ya wakuu wa wilaya walitemwa kutokana na upungufu, ikiwa ni pamoja na madeni mitaani.
Rais alisema baadhi yao walikuwa wakienda baa wanalewa na ili kuwaondoa ilibidi wake zao waitwe kuwachukua. Rais Kikwete alisema hayo jana mjini Dodoma alipokuwa akifungua semina elekezi kwa wakuu wa wilaya 27 wapya walioteuliwa hivi karibuni.
Februari 18 mwaka huu, Rais Kikwete alifanya mabadiliko ya wakuu wa wilaya na kutengua uteuzi wa wakuu wa wilaya 12. Rais Kikwete alisema waliotemwa walikuwapo wenye
upungufu mbalimbali na wengine walikuwa na madeni mitaani huku baadhi
yao wakiwa na tatizo la ulevi kiasi kwamba wakienda baa hulewa kupita
kiasi.
Aliwaasa wakuu wa wilaya wapya kuwa wengine ni wadogo kiumri lazima wafanane na madaraka waliyopewa. “Pale ulipo ni role model (mfano wa kuigwa),
lazima uwe na tabia njema kwa kauli, matendo, nidhamu na uadilifu
usiotiliwa shaka,” alisema.
CHANZO: MWANANCHI

No comments:
Post a Comment