
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande Othman.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Ban Ki-
Moon, amemteua Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande Othman,
kuongoza jopo la kujitegemea la wataalam kuchunguza, na kutathmini
uhalisi wa thamani ya habari mpya, zinazohusiana na kifo cha kutisha, wa
marehemu Katibu Mkuu wa zamani, Dag Hammarskjold na wanachama wengine
aliokuwa ameambatana nao.Uteuzi huo umefanywa na Ki- Moon juzi jijini New York, Marekani,
kufuatia azimio namba 69/246 lililopitishwa na Mkutano Mkuu wa UN,
uliofanyika Desemba 29, mwaka 2014. Azimio hilo lililomtaka Ki-Moon, ateue jopo la wataalamu ili
kuchunguza kuibuka kwa habari mpya zinazohusiana na kifo cha katibu mkuu
huyo wa zamani, kilichotokea mwaka 1961.
Wengine walioteuliwa kuwa wajumbe, ni pamoja na Kerryn Macaulay wa Australia, na Henrik Larsen wa Denmark. Jopo litafanya kazi ya kupitia na kutathmini thamani ya uhalisi wa
habari zilizotolewa kwa katibu mkuu, na tume ya Hammmarskjold, na
rekodi zingine zinazohusiana, au habari zilizotolewa na nchi wanachama,
au vyanzo vingine.
Jopo hilo huru la wataalamu linatarajiwa kuanza kazi yake Machi 30,
na kuwakilisha ripoti yake kwa katibu mkuu, si zaidi ya Juni 30, 2015. Aidha , Azimio hilo lilizihimiza nchi wanachama kutoa rekodi zozote
zilizo chini yao, zinazohusiana na tukio hilo, na kumpatia katibu mkuu
habari zozote juu ya kifo cha katibu mkuu huyo wa zamani.
CHANZO:
NIPASHE
No comments:
Post a Comment