
Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe
Mitandao ya kijamii imeanza kuchukua nafasi na hata kuwa sehemu ya maisha ya kawaida, watumiaji wake hupata taarifa mbalimbali na pia nafasi ya kuanzisha mijadala motomoto.
Hata hivyo, changamoto kubwa iliyopo katika mitandao hiyo ni ugumu wa kudhibiti mijadala, hivyo wakati mwingine taarifa nyingine zinakosa ukweli na kuhitaji vyanzo zaidi ili kuzithibitisha.
Mitandao ya kijamii imeanza kuchukua nafasi na hata kuwa sehemu ya maisha ya kawaida, watumiaji wake hupata taarifa mbalimbali na pia nafasi ya kuanzisha mijadala motomoto.
Hata hivyo, changamoto kubwa iliyopo katika mitandao hiyo ni ugumu wa kudhibiti mijadala, hivyo wakati mwingine taarifa nyingine zinakosa ukweli na kuhitaji vyanzo zaidi ili kuzithibitisha.
Suala la Zitto Kabwe
kushindwa kesi na hatimaye kuvuliwa uanachama na chama chake cha
Chadema, limekuwa sehemu ya mjadala na malumbano makali katika mitandao
ya kijamii.
Ili taarifa iaminiwe na wasomaji, mitandao mingi
ilinukuu akaunti ya ‘twitter’ ya Kituo cha redio cha East Africa
kilichoitoa taarifa ya Zitto kama habari mpasuko. Katika taarifa hiyo, alinukuliwa Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu akitangaza rasmi Zitto kuvuliwa uanachama.
Katika baadhi ya mitandao majibizano kati ya
watetezi wa Zitto na upande wa pili, yalionyesha kama makundi hayo
yangekuwa ukumbini kuna tukio baya lingeweza kutokea kwa upande mmoja
kushindwa kujizuia na kuanzisha mapigano. Hii inatokana na ukweli kwamba mbunge huyo ana
mashabiki wengi kwenye mitandao ya kijamii na pengine ni miongoni mwa
wanasiasa wachache wanaojitokeza hadharani kwenye mitandao na kushiriki
mijadala bila woga.
Kama kuna suala linalohitaji ufafanuzi kutoka kwa
Zitto, mashabiki wake hawalazimiki kusubiri kauli yake kwenye magazeti
kesho yake kwa kuwa hachelewi kutoa maelezo kupitia kwenye akaunti zake
kwenye mitandao. Hata baada ya uamuzi wa Mahakama Kuu iliyotupilia
mbali pingamizi lake la kutaka asijadiliwe na chama chake, baada ya muda
mfupi Zitto aliibuka katika mitandao ya kijamii akitoa ufafanuzi wa
kilichotokea. “Hatukuwa na wito wa Mahakama leo. Jaji
kahamishiwa Tabora. Hatuna taarifa ya Jaji mpya. Mwanasheria wetu
anafuatilia na atatoa maelezo,’’ alisema kupitia mtandao wa Twitter.
Uandishi wake kwa kiwango kikubwa ulikidhi
mahitaji ya watumiaji wa mitandao ya kijamii ambao wengi hupenda kusoma
sentensi fupi fupi na zinazoeleweka kuliko maelezo marefu yenye ajenda
tofauti.
Mwigulu Nchemba aibuka
Suala la kufukuzwa kwa Zitto pia limegusa viongozi mbalimbali
serikalini akiwamo Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba aliyetumia
mtandao wa kijamii wa ‘Jamii Forum’ kuelezea hisia zake kuhusu tukio
hilo.
Katika ujumbe wake mfupi ambao uliibua mjadala
mkubwa kwa wachangiaji, aliandika akisema kuwa amesikitishwa na taarifa
za kuenguliwa kwa Zitto kwenye chama alichoanzia maisha yake kisiasa.
Nikimnukuu zaidi alisema: ‘‘Nakusihi kijana
mwenzangu,mwanasiasa mwenzangu na mchumi mwenzangu kuwa, Taifa
linakuhitaji wakati huu tunapopambana na ufanyaji kazi wa mazoea na
kuleta “mabadiliko kwa vitendo.”Hivyo usikate tamaa Watanzania
watakuhesabia mema kwa yote unayoyafanya kwa ajili ya Taifa letu. Katika mtandao huu ni nadra mwanzisha hoja kubaki
jukwaani kukabialiana na mashambulizi ya mada aliyoanzisha, badala yake
hukaa pembeni na kushuhudia wapambe wenye mitazamo tofauti wakijibizana.
Mwigulu alimtaja mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini
kama mwanasiasa aliyeleta chachu ya mabadiliko kwa vitendo kutokana na
uwezo wake mkubwa na kuwa adhabu yake siyo kumfukuza bali demokrasia
itumike.
Mjadala ulioanzishwa na Mwigulu mpaka leo
haukupata hitimisho kutokana na ukweli kuwa wachangiaji wengi walitaka
kujua sababu za mwanzisha hoja kusikitika badala ya kufurahi na
kumkaribisha kwenye kundi lake. Katika mazingira ya kisiasa, Mwigulu na chama
chake cha CCM walitegemewa wangefurahi kwa kuwa hatua hiyo ilikuwa
inatafsiri kudhoofika kwa chama kikuu cha upinzani (Chadema)na kinyume
chake walionyesha kusikitika.
Mshangao pia ulionyeshwa na mchambuzi wa masuala
ya soka nchini, Edo Kumwembe ambaye kupitia akaunti yake ya Twitter
alijaribu kuhusisha suala hilo na mchezaji bora wa mpira ambaye kila
timu ingependa kuwa naye kikosini.
Alisema kilichomshangaza katika suala hilo ni hata
Chama cha CCM kulalamika. Kwa mtazamo wake alifikiri huo ulikuwa wakati
mwafaka kuona kuwa Chadema inadhoofika na bila kuchelewa wangemsajili
Zitto kwa gharama yoyote kwenye timu yao.
Alijiuliza kwa nini CCM wanahuzunika badala ya
kufurahi huku akioanisha tukio la mchezaji Amis Tambwe alivyoachwa na
timu ya Simba ambaye mpinzani wake Yanga ilimsajili na kumwingiza kwenye
kikosi cha kwanza.
Kwenye ‘Whatsapp’ wazodoana
Kwa watumiaji wa mtandao wa whatsapp picha za
Zitto zilisambaa kama moto wa nyika zikimuonyesha katika matukio tofauti
kuanzia uwezo wake wa kujenga hoja bungeni hadi kwenye majukwaa ya
kisiasa.
Watumiaji wa mtandao huo pia walipata nafasi ya kuangalia video
fupifupi zilizomuonyesha mbunge huyo machachari akishiriki harakati
mbalimbali za kisiasa, ikiwa ni pamoja na msimamo wake wa kusimama
upande wa wanyonge. Tatizo kubwa la mtandao huu kuna picha nyingi za kuchongwa na maneno ya kulishwa. Hata hivyo, kwa mashabiki wa Zitto Kabwe hilo sio
tatizo sana kwao kwani kiongozi huyo wanamjua vilivyo na hata staili ya
uandishi wake mitandaoni inajulikana.
Kama ilivyokuwa katika mitandao mingine hata
watumiaji wa mtandao huu wamejiunga katika makundi, walijadili hoja ya
kufukuzwa kwake kwa mtazamo tofauti na makundi mengi yalionekana
kuwaganyika. Baadhi ya washiriki wa mjadala kupitia mtandao huo
walikosoa uamuzi wa Chadema kumfukuza mwanachama waliyeishi naye kwa
miaka 19, huku wengine wakimuonyesha Zitto kama shujaa mwoga ambaye ni
hatari kumuamini kwenye mstari wa mbele wa mapambano.
Walimtaja kama kiongozi mwenye uwezo wa kujieleza;
mwenye kushawishi ambaye pia ni mtendaji wa kile anachokiamini; kwamba
siyo kama wengine ambao nguvu yao huishia kwenye upigaji kelele
majukwaani.
Pia, katika mtandao huo watumiaji wake walipata
andiko lenye sifa zaidi ya ishirini za Zitto Kabwe kama
zilivyoorodheshwa na mmoja wa mashabiki wake, akimsifia kama kijana
anayesimamia kauli yake bila kujali matokeo mbele ya safari.
Kwa upande wa blogu, ilikosa jipya kuhusu tukio la
kufukuzwa kwa Zitto Kabwe ndani ya Chadema na haikuwa na picha za tukio
la mahakamani zaidi ya kunukuu taarifa kwenye mitandao mingine ya
kijamii. Sifa ya kwanza ya mitandao ya aina hii lazima iwe
na picha za wakati huo ili kikidhi matarajio ya wasomaji. Wengi
walitarajia kuona picha za eneo la mahakamani na jinsi watu walivyokuwa
wanafurahia au kusikitishwa na uamuzi wa Mahakama Kuu.
Hata blogu za kwanza kusambaza taarifa hizo pia hazikuwa na picha yoyote inayotoa taswira ya tukio la siku hiyo mahakamani. Pamoja na mapambano yanayoendelea kwenye mitandao
tofauti ya kijamii, ipo mijadala inayoonekana kubeba sura ya kitaifa
kutokana na historia ya Zitto ndani ya Chadema na mchango wake ndani na
nje ya chama.
Suala la kumpinga Zitto Kabwe kwa hofu ya kuogopa
kukaribisha mabadiliko ya uongozi ndani ya Chadema ni hoja ambayo
kupitia watetezi wake itaendelea kuelea kwenye mitandao ya kijamii kwa
muda mrefu.
CHANZO: MWANANCHI
CHANZO: MWANANCHI
No comments:
Post a Comment