Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) ambao Serikali 
ya Tanzania imeanza kuutekeleza tangu Julai, 2013, umeleta matokeo 
makubwa ambayo yanaelezwa kuwa yatasaidia kukuza uchumi wa nchi. Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa kwenye vyombo vya habari baada ya 
semina liyohusisha viongozi mbalimbali visiwani Zanzibar juzi,  Mtendaji
 Mkuu kutoka Ofisi ya Rais-Usimamizi wa Utekelezaji wa Miradi (PDB) 
inayosimamia utelezaji wa BRN kwa Tanzania Bara, Omari Issa, mafanikio 
hayo yametokana na nidhamu ya utendaji kazi na mfumo uliowekwa na 
serikali.
Katika semina hiyo iliyohudhuriwa na Rais wa Zanzibar, Dk. Ali 
Mohammed Shein, mawaziri, makatibu wakuu na viongozi wengine waandamizi 
wa serikali, Issa alieleza uzoefu wa mwaka mmoja wa utekelezaji wa BRN 
Tanzania Bara. Alisema mafanikio mengine mbali na nidhamu ya utendaji na mfumo 
uliowekwa ya BRN kwa Tanzania Bara, yametokana pia na vipaumbele 
vichache vinavyogusa sekta muhimu kwa taifa.
Alitaja baadhi ya mafanikio ambayo yamepatikana kupitia mfumo huo 
wa BRN kwa Tanzania Bara kuwa ni sekta ya maji, uchukuzi na nishati. Katika semina hiyo, mtaalam ambaye pia ni Waziri Katika Ofisi ya 
Waziri Mkuu wa Malaysia na Mkuu wa Kitengo cha Utekelezaji wa Miradi ya 
Kipaumbele nchini humo (Pemandu), Dk. Idris Jalla, alisema serikali 
nyingi duniani zina mipango mingi mizuri, lakini utekelezaji wake 
umekuwa ni tatizo.
     CHANZO:
     NIPASHE
    


No comments:
Post a Comment