Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Wizara ya Habari, Vijana, Concilia Niyibitanga
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana, imevikopesha Sh. 415,919, 000 kwa
vikundi vya vijana 67 wa Halmashauri 25 za Tanzania Bara.
Akizungumza na NIPASHE, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Wizara
hiyo, Concilia Niyibitanga, alisema mikopo hiyo imetolewa kwa lengo la
kuwasaidia vijana kupata mikopo yenye masharti nafuu ili kuwajengea
uwezo kiuchumi kwa kuanzisha miradi yao itakayowawezesha kujitegemea na
kukuza uchumi wa nchi.
“Fedha za mfuko wa Maeandeleo ya Vijana ni kwa ajili ya vijana wote
nchini, kila kijana anayo haki ya kunufaika na na mkopo kutoka mfuko
huu,” alisema Concilia.
“Vijana wanatakiwa kukopa na kurejesha tofauti na wengine wanavyohusisha
fedha hizi na masuala ya kisiasa, wakidhani ni zawadi,” alisema.
Niyibitanga alisema kutokana na changamoto zilizojitokeza hususani
katika urejeshaji na usimamizi wa mikopo iliyotolewa, Serikali iliamua
kubadilisha utaratibu wa utoaji mikopo hiyo na kufuata utaratibu mpya
ambao huhusisha miradi iliyoidhinishwa na wizara, mikoa na halmashauri.
Aidha, alisema wizara bado ipo katika mchakato wa kuhamasisha vijana kujiunga katika vikundi vya ujasiriamali kusajili vikundi vyao na hatimaye vikundi hivyo kujiunga katika SACCOS za vijana huku akisisitiza ni mojawapo ya kigezo cha kikundi kupata mkopo. Aliongeza kuwa katika mwaka huu wa fedha, Serikali imetenga Sh. bilioni sita kwa ajili ya mfuko huo.
Alifafanua kuwa mfuko huo unakabiliwa na changamoto mbali mbali zikiwamo fedha zilizotengwa hazitoshelezi mahitaji ya vijana, mwamko mdogo wa urejeshaji mikopo kwa wakati na maandiko ya miradi mingi kutokidhi vigezo vya kukopesheka.

CHANZO:
NIPASHE

No comments:
Post a Comment