Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), Jaji mstaafu Damian Lubuva.
Shangwe, nderemo na vifijo, vilitawala katika mji wa
Chato na viunga vyake baada ya mgombea wa urais kupitia Chama Cha
Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli, kutangazwa rasmi kuwa mshindi wa
kinyang’anyiro cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), Jaji mstaafu Damian
Lubuva, alimtangaza Dk. Magufuli kuwa mshindi halali wa nafasi hiyo
jijini Dar es Salaam jana baada ya kupata kura nyingi kuliko wagombea
wenzake. Kwa matokeo hayo, Dk. Magufuli atakuwa Rais wa awamu ya tano.
Watangulizi wa Dk. Magufuli ni hayati Mwalimu Julius Nyerere, Ali Hassan
Mwinyi, Benjamin Mkapa na Rais anayemaliza kipindi chake, Jakaya
Kikwete.
Shamrashamra za wakazi wa Chato zilisababisha shughuli mbalimbali
za kijamii kusimama na wananchi kuingia mitaani kushangilia ushindi wa
Dk. Magufuli.
Wakati wakishangilia ushindi huo, wananchi walisikika wakiimba
“aliselema, alija huku baadhi yao wakiwa wamebeba bendera za CCM na
waendesha bodaboda wakipita mitaani wakiziendesha kwa mbwembwe. “Nina
furaha isiyo kifani kusikia Dk. Magufuli ameibuka kidedea,” alisema kwa
kifupi, Mary Mathayo, mkazi wa mjini hapa.
Kwa upande wake, Michael Andrew, alisema anajivunia kupata rais
anayetoka katika wilaya aliyopo na kwamba anatarajia kuona maendeleo
makubwa zaidi kutoka kwa Rais mpya wa awamu ya tano ambaye ni mzaliwa wa
Wilaya ya Chato.
CHANZO:
NIPASHE

No comments:
Post a Comment