Jaji Mkuu wa Zanzibar, Omar Othman Makungu, jana
aliwaapisha wasuluhishi na waamuzi watakaoshughulikia migogoro ya kazi
Zanzibar.Walioapishwa ni Sisahau Rished Faki na Nemshi Abdallah. Akizungumza baada ya kuwaapisha, Jaji Makungu alisema uteuzi huo
utasaidia kushughulikia malalamiko ya wafanyakazi katika Mahakama ya
Kazi.
Alisema malalamiko hayo yatashughulikiwa kwa ufanisi zaidi ili haki itendeke kati ya mlalamikaji na mlalamikiwa. Aliwataka wasuluhishi hao kutenda haki katika majukumu yao ya kazi bila kuwa na upendeleo.
Kamishna wa kazi Zanzibar, Kubingwa Mashaka Simba, alisema jumla ya
malalamiko 102 ya wafanyakazi yameripotiwa kwa mwaka 2013/3014 kati ya
hayo, 59 yalipatiwa usuluhishi.
Alisema kuwa migogoro mingi wanayopokea kwa wafanyakazi ni tuhuma
za wafanyakazi kufukuzwa kazi, wizi na kukatishwa mikataba kazini.
Waziri wa Kazi na Utumishi wa Umma, Haroun Ali Suleiman, alisema
Serikali ya Zanzibar imekuwa ikichukua hatua mbalimbali za kutatua
migogoro ya wafanyakazi.
CHANZO:
NIPASHE

No comments:
Post a Comment