Social Icons

Pages

Tuesday, March 17, 2015

TAMASHA LA KISWAHILI KUFANYIKA DAR

Waziri wa Habari Utamaduni Vijana na Michezo, Dk Fenella Mukangara akimsikiliza Rais wa tamasha la kimataifa la Lugha na Utamaduni, Ali Akkiz.

Tanzania itakuwa mwenyeji wa Tamasha la Kimataifa la Lugha na Utamaduni litakaloandaliwa na Shirika la Kilimanjaro Dialogue Institute kuanzia tarehe 21-22 Machi 2015. Tamasha hili litafanyika katika Ukumbi  wa Mwalimu J.K. Nyerere jijini  Dar es Salaam.
Rais wa Shirika la Kilimanjaro Dialogue Institute Ali Akkiz aliueleza uongozi wa Wizara ya Habari, Utamaduni , Michezo na Vijana ulioongozwa na Mhe Dr Fenella Mukangara, jinsi walivyojiandaa kufanikisha tamasha hilo.
Ali Akkiz alifafanua kuwa wawakilishi 18 kutoka nchi mbalimbali duniani  watahudhuria tamasha hilo. Nchi hizo ni pamoja na Tunisia, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Romania, Nigeria, Kenya,  Kongo (DRC), Afrika Kusini, Iraq, Uganda, Mozambique na Thailand.
Katika kikao kilichofanyika Makao Makuu ya Wizara, viongozi waliohudhuria kikao hicho ni Waziri Dr Fenella Mukangara, Naibu Katibu Mkuu Prof Elisante Ole Gabriel na Mkurugenzi Msaidizi wa Utamaduni Bi Lilliy Beleko.

CHANZO: MWANANCHI

No comments: