Prisca Cosmas na mwanae
Ni kama ndoto lakini ni kweli nimepatwa na sitofahamu kuhusu hatima ya maisha ya watoto wangu watatu wenye ulemavu wa ngozi (albino). Sijui nikimbilie wapi ili niokoe maisha yao. Mungu simama pamoja na watoto wangu kwani nao wana haki ya kuishi.”
Hiyo ni kauli ya Prisca Cosmas ambaye sasa yupo katika Hospitali ya Rufaa Mbeya, akimuuguza mtoto wake Baraka Cosmas (6) , mwenye ulemavu wa ngozi aliyekatwa kiganja cha mkono siku chache zilizopita.
Ni kama ndoto lakini ni kweli nimepatwa na sitofahamu kuhusu hatima ya maisha ya watoto wangu watatu wenye ulemavu wa ngozi (albino). Sijui nikimbilie wapi ili niokoe maisha yao. Mungu simama pamoja na watoto wangu kwani nao wana haki ya kuishi.”
Hiyo ni kauli ya Prisca Cosmas ambaye sasa yupo katika Hospitali ya Rufaa Mbeya, akimuuguza mtoto wake Baraka Cosmas (6) , mwenye ulemavu wa ngozi aliyekatwa kiganja cha mkono siku chache zilizopita.
Tukio la Baraka kukatwa kiganja lilitokea usiku wa
manane kuamkia Machi 6 katika Kijiji cha Kipeta , Bonde la Ziwa Rukwa,
wilayani Sumbawanga Vijijini .
Prisca, ambaye ni mama wa watoto wanne anasimulia
kwa uchungu kuwa siku ya tukio, licha ya mtoto wake kukatwa kiganja,
naye alipigwa rungu kichwani lililosababisha apoteze fahamu pamoja na
kupata jeraha kubwa. Mama huyo anasema kuwa katika uzazi wake ana watoto wanne wakiwamo watatu wenye ulemavu wa ngozi.
Anabainisha kuwa mbali na Baraka watoto wengine wenye ulemavu huo ni Hosia Cosmas (4) na Jafari Cosmas (2). “Ukatili huo ulitokea saa 7 usiku. Nilikuwa
nafungua mlango kwenda kujisaidia. Nilipofungua mlango, ghafla nilisikia
sauti ya mtu ikimuamuru kukaa kimya, hali ambayo ilinishtua.
Katika uvamizi huo nilijitahidi kupambana kumwokoa
mwanangu, lakini ilishindikana. Yote namwachia Mungu,” anasema Prisca
na kuongeza: “Sikupenda kuzaa watoto walio na ulemavu wa ngozi
ni mipango ya Mungu, inaniuma sana na natambua mimi ni wa kuishi maisha
ya hofu kila siku. Kuna wakati naomba giza lisiingie.” “Nipo njiapanda, sijui watoto hawa wenye ulemavu
nitawalea vipi? Naomba msaada wa ulinzi kutoka kwa Serikali, majirani na
wasamaria,” anasema Prisca na kusisitiza: “Nina hofu hata kurejea
nyumbani kwangu kwani naamini watu hao wabaya watarudi kuhatarisha
maisha yetu.”
Prisca ni mkazi wa Kijiji cha Kipeta, aliolewa na
mwanaume anayemtaja kwa jina la Cosmas. Yeye ni mke wa kwanza kwa
mwanaume huyo, ambaye sasa ameoa mke wa pili.
Kikwete ateta na viongozi
Kauli za viongozi
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Stella Manyanya anasema
kuwa tukio hilo ni la aibu kwa Mkoa hata Taifa na kwamba ni lazima
wahusika watasakwa popote walipo. Anaeleza kuwa Rais Jakaya Kikwete alishatoa agizo,
hivyo wakuu wa mikoa lazima wahangaike kwa kutumia Kamati za Ulinzi na
Usalama wanazoziongoza katika mikoa yao kukomesha uonevu huo.
“Wakati umefika kwa wakuu wa mikoa wote na kamati
za ulinzi na usalama kukutana na kujadili nini kifanyike ili kutokomeza
vitendo hivyo vya kikatili dhidi ya wenzetu wenye ulemavu wa ngozi
albino,’’ anasema.
Akiwa Hospitali ya Rufaa Mbeya, Manyanya anasema
kuwa ni jambo la kushangaza kuendelea kwa matukio hayo kwani hivi
karibuni Rais Jakaya Kikwete alishatangaza mapambano dhidi ya matukio ya
mauaji, kukatwa viungo vya watu wenye ulemavu wa ngozi.
“Ndugu zangu, watu wanaofanya vitendo hivi
mnawajua, wanakaa katika mitaa, vijiji na vitongoji. Sasa ni wakati wa
kuondoa hofu, mtangulizeni Mungu muwafichue na sisi Serikali
hatutavumilia vitendo hivi,’’ anasema. Naye Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro anasema
kuwa wakati sasa umefika kwa wananchi kutambua kwamba ni jukumu la wote
kupambana dhidi ya wahalifu na kwamba ushirikiano wa dhati unahitajika
zaidi .
Chama cha Albino Mbeya
Katibu wa Chama cha Watu Wenye Ulemavu wa Ngozi,
Mkoa wa Mbeya, William Simwali anaishauri Serikali kutafuta njia ili
kumsaidia mwanamke huyo kulea watoto wake watatu. Anashauri Serikali kuwajengea kituo maalumu cha kuishi watu wenye ulemavu wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini.
Anasema kuwa licha ya Serikali kupiga marufuku
waganga wanaopiga ramli, lakini bado wapo wanaendesha shughuli zao kwa
vificho akaongeza kwamba Serikali kupitia polisi haina budi kufanya
msako wa nyumba kwa nyumba ili kuwabaini na kuwafikisha wahalifu hao
kwenye mikono sheria.
Kikwete ateta na viongozi
Wiki mbili zilizopita Rais Kikwete aliwaeleza viongozi wa Albino
waliomtembelea Ikulu jijini Dar es Salaam ambao walioongozwa na
Mwenyekiti wao, Ernest Kimaya kuwa; “Mauaji haya yanaisikitisha Serikali
na kuifedhehesha sana”. “Msidhani hatufanyi lolote, tunafanya juhudi kubwa na mbalimbali lakini imefikia wakati tuongeze juhudi hizo,” alisema Kikwete.
Katika kikao hicho viongozi hao, walisoma risala
ambayo imetoa kilio chao na mapendekezo yao kwa Serikali na hatimaye
ikaafikiwa kuwa na haja ya kuunda kamati ya pamoja ambayo itajumuisha
Serikali, viongozi wa Albino, viongozi wa waganga wa jadi na wadau wote
wakuu katika suala hili ili kupata mapendekezo na mkakati wa pamoja
ambao hatimaye mauaji haya kukomeshwa kabisa nchini.
Rais Kikwete alisema mauaji hayo hayafanywi na
Serikali bali watu ambao wako katika jamii kwa kushirikiana na waganga
wa jadi na watu wengine wenye tamaa mbalimbali katika jamii hivyo na
kwamba ni lazima yakomeshwe. “Kwenye familia, jamii na hatimaye vyombo vya
ulinzi na usalama na hilo ndiyo jukumu kubwa ambalo Serikali inapaswa
kulisimamia na tutalisimamia kwa ushirikiano wa pamoja,” aliahidi.
“Mauaji haya yanaisikitisha Serikali na
kuifedhehesha sana, msidhani hatufanyi lolote, tunafanya juhudi kubwa na
mbalimbali lakini imefikia wakati tuongeze juhudi hizo”alisema Rais. Rais alisisitiza kuwa kamati hiyo ya pamoja
itaweka mikakati ya kuwabaini wale wote wanaohusika kuanzia wakala,
waganga na hatimaye wale wanaonufaika na viungo vya walemavu hao.
Pia, aliahidi kuwa Serikali itasaidia familia na
wahanga wa vitendo vya mauaji kwa hali na mali ili waweze kujimudu na
pia kuwapa ushauri nasaha ili kuondokana na majonzi yanayosababishwa na
vitendo hivyo kwani vinawaletea waathirika na watu wanaoishi nao
mfadhaiko na msongo wa mawazo katika jamii.
Viongozi hao walitoa kilio chao kwa Serikali
kuziangalia na kuzimulika taasisi zisizo za kiserikali ambazo pamoja na
kujipambanua kuwa zinatetea haki za Albino nchini bado hazina mkakati wa
pamoja na hazipo wazi kwa walengwa hapa nchini.
CHANZO: MWANANCHI
CHANZO: MWANANCHI

No comments:
Post a Comment