
Serikali imepongeza jitihada za Mwenyekiti Mtendaji
wa IPP, Dk. Reginald Mengi, katika kuwezesha Vikundi vya Kuweka Fedha na
Kukopa (SACCOS) hasa vya wanawake na vijana kwa lengo la kufanikisha
mpango wa maisha bora kwa kila Mtanzania.
Naibu Waziri wa Fedha, Adam Malima, alisema serikali inatambua na
kuthamini jitihada hizo na alihamasisha wafanyabiashara wengine kufuata
nyayo za Dk. Mengi. Waziri Malima, alikuwa akijibu swali la nyongeza la Diana Chilolo
(Viti Maalumu-CCM), aliyeitaka serikali kupongeza jitihada za baadhi ya
wafanyabiashara wanaosaidia wananchi, akitoa mfano wa Dk. Mengi,
aliyemuelezea kwamba amekuwa mstari wa mbele katika kusaidia SACCOS hasa
za wakina mama na vijana.
”Serikali ipo tayari kumpongeza mfanyabiashara huyu ambaye amekuwa
msaada mkubwa kwa Watanzania, pamoja na kuhamasisha wafanyabiashara
wengine, kubeba jukumu la kuwezesha SACCOS za akinamama na vijana kwa
lengo la kuwezesha kufikia mpango wa serikali wa maisha bora kwa kila
Mtanzania?” alihoji Chilolo.
Akijibu swali la msingi lililoulizwa na Hussein Nassor Amar
(Nyang’wale) ambaye alitaka kufahamu sababu za serikali kukopesha fedha
SACCOS za mijini tu huku za vijijini zikikosa fursa hiyo, alisema katika
bajeti ya serikalini, hakuna fungu la fedha kwa ajili ya kukopesha
vyama hivyo.
“Hata hivyo wapo wadau wengi wanaoingia katika makubaliano maalumu
na SACCOS, kisha kuziwezesha serikali ilishajiondoa katika kufanya
biashara na hivyo haijatengeneza mpango wa kukopesha taasisi yoyote
ikiwamo SACCOS,” alieleza Malima
CHANZO:
NIPASHE

No comments:
Post a Comment