Tangu kuingia kwa miatandao ya kijamii nchini
vijana wengi wamepata nafasi ya kuituma au kupokea ujumbe mfupi, picha
na video; kwa njia rahisi zaidi kuliko ilivyokuwa miaka 20 iliyopita.
Watumiaji
wengi wa huduma hiyo hupendelea zaidi mitandao inayowawezesha kutuma
ujumbe wa siri kwa njia rahisi, mara nyingi watakavyo na kwa gharama
ndogo. Kati yao, lipo kundi la wanafunzi linalopendelea kuwasiliana kwa
njia ya kuandikiana ujumbe wa maandishi na kutumiana picha.Kwa mujibu wa takwimu za Machi mwaka huu za Kampuni ya Utafiti ya Statista ya Marekani, mtandao wa Facebook ndiyo unaoongoza kwa kuwa na watumiaji wengi, ukifuatiwa na mtandao wa WhatsApp.
Mitandao mingine na idadi ya watumiaji wake kwenye mabano ni Qzone (watu milioni 629), Facebook Messenger (watu milioni 500), WeChat (watu milioni468), LinkedIn (watu milioni 347), na Twitter (watu milioni 288). Pamoja na kuwa Facebook inatawala orodha ya watumiaji wa mitandao hiyo, wataalamu wa masuala ya teknolojia ya mawasiliano wanasema kuwa miaka michache ijayo vijana wataanza kukimbilia mitandao mingine yenye ‘ladha’ tofauti.
Baadhi ya mitandao hiyo ni pamoja na Kik Messenger, ooVoo na WhatsApp inayowawezesha watumiaji wake kutuma ujumbe kwa urahisi. Kundi la vijana wanaopenda kutuma habari mbalimbali mitandaoni litalazimika kujikita kwenye mitandao ya Instagram, Tumblr, Twitter na Vine.
Kundi jingine ni la vijana wanaopenda kutuma ujumbe wa siri kwa rafiki au wapenzi wao. Kundi hili linavutiwa zaidi na mitandao ya Secret-Speak Freely, Snapchat, Whisper na Yik Yak.
Japokuwa uongozi wa Facebook umekuwa ukijaribu kuja na mbinu mpya kila siku ili kuendelea kuwashikilia wateja wake, bado msukumo wa kizazi kipya kujaribu mambo mapya unabaki kuwa uchaguzi pekee.
Kundi la mwisho ni la vijana wanaotumia muda wao
mwingi kwa ajili ya kuchati na kupeana miadi mtandaoni. Kundi hili
linavutiwa na mitandao ya MeetMe, Omegle, Skout na Tinder.
Mwanafunzi wa mwaka wa tatu katika Chuo Kikuu cha
Tumaini, Dar es Salaam Sunday Elisaria, anasema teknolojia ya
mawasiliano ya simu imeleta matatizo kwa wanafunzi katika nchi za Afrika
kuliko ilivyotarajiwa.
Elisaria anasema kama mwanafunzi angetumia simu
kama chombo muhimu cha kumsaidia kupata taarifa za masomo,
wasingelalamikia ukosefu wa vitabu uliopo katika shule na vyuo nchini.
“Sasa badala ya mwanafunzi kutumia mtandao wa
‘google’ kutafuta taarifa za kitaaluma, muda mwingi anachati na kutuma
picha kwenye ‘Facebook’,” anasema Elisaria.
Kwa mujibu wa mtandao wa ‘Common Sense’, wazazi
wanatakiwa kuelewa kuwa mtandao wa ‘Kik Messenger’ unaruhusu vijana
kutuma ujumbe bure bila kikomo kwa haraka.
Watumiaji wa mtandao wa ‘ooVoo’ wanafurahia
kuangalia picha za video bure, huku mtumiaji akiruhusiwa kuchati na watu
hadi 12 bure.
Mtandao wa kijamii ambao pengine ndio ‘habari ya
mjini’ hivi sasa wa ‘WhatsApp’, unamwezesha mtumiaji kutuma ujumbe,
sauti, video na picha kwa mtu mmoja au wengi. Moja ya masharti ya
‘WhatsApp’ ni kuwa mtumiaji lazima awe na umri wa miaka zaidi ya 16.
Mwanafunzi wa Shule ya Sheria ya Chuo Kikuu cha
Dar es Salaam, Edna John anasema wanafunzi wanaotumia ‘Facebook’
wameanza kuvutiwa na mtandao wa kijamii wa ‘Instagram’ kwa kuwa
unamwezesha mtumiaji kupiga picha, kuzihariri na kuziweka mtandaoni. Pia
unamwezesha mtumiaji kuweka video yenye sekunde 15. ‘Twitter’ inamwezesha mtumiaji kutuma ujumbe mfupi
wa herufi 140. Mara nyingi hutumiwa na watu wazima ambao hupendelea
kutuma ujumbe wa wazi, ingawa inawezekana pia kutuma ujumbe wa siri.
Mitandao hatari kwa vijana
Mitandao ya ‘Secret-Speak Freely’, ‘Snapchat’,
‘Whisper’ na ‘Yik Yak’, inatajwa kuwa ni hatari kwa vijana kwa sababu
inawaruhusu kutumiana ujumbe wa siri au kutamka maneno yoyote
wanayoyataka wakiwa na uhakika kuwa hakuna atakayewagundua.
Wakati mwingine katika mtandao huo, watumiaji husimulia habari
za matukio ya kushangaza na kushtua au kukiri kutenda jambo fulani bila
mtu yeyote kujua ni nani anayezungumza.
Mtaalamu wa masuala ya mitando, Abel Chengula
anasema kama wazazi au walezi wasipojua mtandao gani watoto wake
wanapenda kuingia, inaweza kuchangia ongezeko la mmomonyoko wa maadili.
“Baadhi wa wanafunzi wanachelewa kulala kwa sababu
ya kuchat na watu wasiojulikana, wengine wamejikuta wakipata mimba
baada ya kupata marafiki kwenye mtandano na kushawishika kufanya ngono,”
anasema. Anasema kwa hapa nchini, baadhi ya watu wamejikuta
picha zao zimewekwa kwenye mitandao hiyo bila idhini yao, huku nyingine
zikionyesha wakiwa utupu.
‘MeetMe’ ni mtandao unaowezesha mtuamiaji kuchat
na mtu yeyote atakayekutana naye mtandaoni. Unatumika kwa ajili ya
kuchochea urafiki na ushawishi. “Kitendo cha kuwa mtandao huru unaomruhusu yeyote kuchati na wewe, kinaongeza hatari,” inasema sehemu ya taarifa ya Statista.
Kabla ya kujiunga na mtandao huo, mhusika anatakiwa kujaza fomu kwa kujibu maswali yaliyoorodheshwa.
Mtandao wa ‘Omegle’ unatajwa kuwa hatari kwa
vijana hasa wanafunzi kwa kuwa unawakutanisha kwa njia ya ujumbe mfupi
wa maneno au video watu wawili wasiofahamiana.
Inaelezwa kuwa kitendo hicho kinawavutia vijana
wadogo na kuwatumbukiza katika uhusiano na watu wasiowajua vyema. Pia,
mtandao huo unaweza kuruhusu watu kuona mazungumzo iwapo wawili hao
watakubaliana kufanya hivyo. “Hakuna usajili wowote unaohitajika. Huu siyo
mtandao wa watoto ni maalumu kwa watu wazima wanaotafuta wapenzi,”
unasema mtandao wa ‘Common sense media’.
Unaongeza: “Wanachotakiwa kujua wazazi ni kwamba watu watu wawili wasiofahamiana wanakutanishwa, kwa sababu hawafahamiani.”
Mtandao wa ‘Skout’ unawawezesha watumiaji vijana
wadogo kuingia (sign up) kama watu wazima, jambo linalowawezesha
kushiriki mijadala kama wanachama wengine. ‘Skout’ ni maalumu kwa ajili
ya kutafuta wachumba. “Mtandao huu ni mzuri tu kwa mtoto wako iwapo atasimamiwa wakati
anapoutumia. Kutokuwa na sehemu ya kuthibitisha umri kwenye mtando huu
kinampa mtoto nafasi ya kusema ana miaka 18,” unaongeza mtandao huo.
Mwanasaikolojia raia wa Israel aliwahi kusema: “Watoto ni kama sarufi iliyoloa, kitu chochote kitakachowaangukia kinaweza kuwaathari.
CHANZO: MWANANCHI
Mwanasaikolojia raia wa Israel aliwahi kusema: “Watoto ni kama sarufi iliyoloa, kitu chochote kitakachowaangukia kinaweza kuwaathari.
CHANZO: MWANANCHI
No comments:
Post a Comment