
Mwemyekiti wa Jukata, Deus Kibamba.
Jukwa la Katiba Tanzania (Jukata), limesema kura ya
maoni ya kuipigia Katiba inayopendekezwa iahirishwe hadi uchaguzi mkuu
wa mwaka huu utakapofanyika ili kujenga muafaka kati ya vyama vya siasa
na kufanya maandalizi ya kina ya upigaji kura hiyo.
Upigaji kura hiyo unatarajiwa kufanyika Aprili mwaka huu.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Mwemyekiti wa
Jukata, Deus Kibamba, sababu kumi zinatosha kuwa hoja kuu za kuahirisha
mchakato huo, ikiwamo kutekeleza makubaliano kati Rais na vyama vya
siasa.Kibamba anazitaka sababu zingingine kuwa maaandalizi duni ya kura ya maoni pamoja na Bunge Maalum la Katiba ambalo lilishindwa kufikia muafaka na maridhiano. Kibamba aliongeza kuwa uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika Desemba 2014, ulikuwa na dosari nyingi na kusababisha fujo na vurugu kutokana na maandalizi yasiyoridhisha.
“Idadi ya wapiga kura ilikuwa ndogo katika uchaguzi wa serikali za mitaa, tunapaswa kujifunza kutokana na makosa ya siku za nyuma na pia tulikiuka makubaliano ya vyama vya Siasa na Mheshimiwa Rais yaliyofanyika Dodoma kuwa uchaguzi wa serikali za mitaa uahirishwe hadi mwaka huu ili kufanya maandalizi,” alisema.
Pia, ilieleza kuwa Watanzania hawajapata nakala ya katiba inayopendekezwa ili kuisoma kabla ya kufaya maamuzi ya kupiga kura hiyo. Alisema Watanzania wanahitaji kupata nakala za rasimu ya Katiba ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Katiba ya mwaka 1977 toleo la 2005 pamoja na ya Zanzibar ya mwaka 1984 toleo la 2010.
CHANZO:
NIPASHE

No comments:
Post a Comment