Mahakama ya Mombasa
imewahukumu wanaume wanne raia wa Kenya kifungo cha miaka 40 jela kila
mmoja, kwa kuwakuta na hatia ya kumuua mtafiti wa madini raia wa
Scotland huko Taveta, karibu na mpaka wa Kenya na Tanzania.
Watu waliohukumiwa ni Wachimba-migodi huko kwao kaunti ya Taita
Taveta, walioshtakiwa miaka mitano iliyopita kwa kumuua Mskochi Campbell
Rodney Bridges mtaalamu wa Madini. Mahakama kuu mjini Mombasa
imewahukumu watu hao baada ya ushahidi kuonesha walikuwa na ubaguzi,
wakidai kuwa raia wa kigeni alifaidi kutokana na madini fulani yaliyo
eneo lao.
Jaji Maureen Odero aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo alisema “Mohamed
Dadi, Alfred Njuruka, Samwel Mwachala na James Chacha, walihusika na
mauaji ya Campbell Rodney Bridges,raia wa Scotland”. Watuhumiwa
walishtakiwa kumuua Bridges raia Agosti mwaka 2009 eneo la Kwambaga
Mwasui “Ranch” kaunti ya Taita Taveta.
Mahakama iliwapata na hatia Wachimba-migodi hao, baada ya kusikiliza mashahidi kwa miaka Mitano. Polisi walikuwa wamewashtaki watu nane lakini wanne wakaachiwa huru,
akiwepo mtu aliyetejwa kuwa jamaa wa mbunge wa Taveta Naomi Shaban.
Wakati kesi hiyo ilipokuwa ikisikilizwa Bi. Shaban alimtetea “mjomba
wake” kwa kuwasilisha kitabu mahakamani, kuonyesha kwamba alikuwa
amemtembelea Nairobi wakati mauaji ya Bridges yaliporipotiwa kutekeelzwa
huko Taveta. Marehemu Bridges Rodney aliishi Kenya kwa Takriban miaka 35, tangu
alipozuru mwaka wa 1974, na kusaidia katika utafiti wa madini kaunti ya
Taita Taveta.
CHANZO: VOA

No comments:
Post a Comment