Wabunge wa Kenya waliweza kupitisha mswada mpya wenye utata, juu ya
usalama baada ya kupigana magumi bungeni siku ya Jumatano, katika kikao
maalum kilichokuwa na mabishano makali. Mungano
unaotawala wa Jubilee umekuwa ukihimiza kupitishwa kwa mswada huo kama
njia ya kuiwezesha taifa hilo kukabiliana na ongezeko la kitisho cha
ugaidi.
Mbunge Muthoni Wahome anasema, "wakenya
wanahamu ya kuimarisha usalama, kwa sababu wametaabika sana kama nchi,
hatutalegeza kamba. Kama wanajubilee na watu wenye nia njema tutapitisha
mswada leo."
Wabunge
wa upinzani wanabisha kwamba vipengele vya mswada huo utawapokonya
waananchi haki zao msingi waloweza kujinyakulia baada ya kupitishwa kwa
katiba mpya, na kudai hawakupata muda wa kutosha kuujadili mswada.
Alfred Keter mbunge mwengine anasema, "ninataka
kuona baraza la wawakilishi lililoungana ili tuweza kupitisha mswada
mzuri zaidi. Na haijalazimu kuharakisha mambo, hatuna haja ya kumaliza
sasa, hii si mwisho wa dunia, tumewapoteza Wakenya wengi na tunataka
sharia za kudumu. Hebu tupeane muda.
Mbunge mmoja asiyetaka kutajwa anasema mswada ulopitishwa umefanyiwa marekebisho muhimu na hauko sawa na ule ulopendekezwa.
Mabalozi
wa mataifa 9 nchini Kenya akiwemo balozi wa Marekani, walitoa taarifa
Jumatano kueleza wasi wasi wao kuhusiana na mswada huo. Wanasema
wanaunga mkono mipango ya kuimarisha usalama lakini sio kwa kuvuruga
haki za binadamu.
Kabla
ya kikako cha asubuhi cha bunge, usalama uliimarishwa katika njia zote
za Nairobi na kuna watu walokamatwa walipojaribu kuandamana kupinga
kupitishwa kwa mswada huo.
CHANZO: VOA


No comments:
Post a Comment