
Watumiaji wanaotegemea meli ya Mv
Victoria juzi walipata adha ya usafiri baada ya kusitishwa kwa safari ya
kuelekea Mwanza hatua iliyochukuliwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri
wa Majini na Nchi Kavu (Sumatra)kwa madai kwamba ilitoroshwa bila
kukaguliwa.
Ofisa Mfawidhi wa mamlaka hiyo, mkoani Kagera,
Kapteni Alex Katama alisema awali, meli hiyo ilizuiliwa Mwanza kwa ajili
ya matengenezo na kwamba haikufanyiwa ukaguzi kabla ya kuruhusiwa na
akisisitiza kuwa meli hiyo bado mbovu.
“Ilifika Bukoba ikitumia injini moja bila ruhusa
ya mamlaka, tutaendelea kuizuia mpaka itakapofanyiwa ukaguzi na
kujiridhisha, kosa lililofanyika halitakiwi kujirudia mara ya pili,’’
alisema Kapteni Katama
Hadi inazuiliwa, ilikuwa ikijiandaa kwa safari hiyo ya Mwanza na tayari mizigo ilikuwa imeshapakiwa.
Akizungumza kwa simu juzi, Meneja Masoko wa
Shirika la Huduma za Meli, Obed Tirugumila alisema mv Victoria
ilifanyiwa matengenezo Mwanza lakini haikufanyiwa majaribio na maofisa
wa ukaguzi wa Sumatra akidai kuwa walisema hawana nafasi.
Tirugumila alisema waliamua kufanya majaribio kwa
kwenda Bukoba wakiwa na abiria na kufika salama, lakini baadaye
walipokea amri ya Sumatra ikiizuia meli hiyo kusubiri ukaguzi.
Kutokana na hatua hiyo, baadhi ya wafanyabiashara
waliandamana hadi kwa Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Ziporah Pangani
kulalamikia kusitishwa ghafla kwa safari hiyo wakidai kwamba itawapa
hasara ya kuharibika mazao yao. Hata hivyo, Pangani aliwataka wafanyabiashara hao kurudi katika ofisi za meli hiyo akisema wanapaswa kutii agizo la Sumatra.
CHANZO: MWANANCHI
CHANZO: MWANANCHI
No comments:
Post a Comment