Maafisa, wakaguzi na askari wa jeshi la polisi
nchini, wametakiwa kudumisha nidhamu, haki, na kuwaheshimu wananchi wa
rika zote bila ya kujali dini, rangi au itikadi za kisiasa.
Wito huo ulitolewa na Mkuu wa Chuo cha Polisi Dar es Salaam, SACP Ali
Lugendo, wakati akizungumza na wanafunzi wa mafunzo ya uofisa (Mrakibu
Msaidiizi wa Polisi) na wa cheti na stashahada ya Sayansi ya Polisi
kutoka mikoa mbalimbali.Kamanda Lugendo alisema kuwa pamoja na kufundisha masomo ya sheria na haki za binadamu, kazi kubwa inayofanywa na chuo chake ni kusisitiza nidhamu kwa kila afisa na askari wanaofika chuoni hapo.
Alisema nidhamu ni somo la kwanza analofundishwa askari mafunzo ya awali kwani ni msingi wa kwanza kwa majeshi yote duniani. “Hakuna jeshi lolote duniani, likiwemo jeshi letu la polisi ambalo haliendeshi kwa misingi ya nidhamu,” alisema na kuongeza bila nidhamu hakuna jeshi.
Kwa upande wake, Afisa Mkuu wa nidhamu wa chuo cha Polisi Dar es
Salaam (Dar es Salaam Police Academy) SSP Mussa Loyd, aliwataka maafisa
hao kuwa kioo cha jamii na kuwatendea haki wananchi bila upendeleo
wakati wote wanapokuwa kazini.
Alisema mbali ya kuzuia vitendo vya kihalifu, kushuku, kupeleleza na kuwakamata watuhumiwa, kazi kubwa ya jeshi hilo ni kuhakikisha kila askari anatenda haki kwa kila anayemhudumia bila ya ubaguzi au kumuonea mmoja wao.
Alisema mbali ya kuzuia vitendo vya kihalifu, kushuku, kupeleleza na kuwakamata watuhumiwa, kazi kubwa ya jeshi hilo ni kuhakikisha kila askari anatenda haki kwa kila anayemhudumia bila ya ubaguzi au kumuonea mmoja wao.
CHANZO:
NIPASHE

No comments:
Post a Comment