Mmiliki wa Kampuni
ya Kufua Umeme ya IPTL, Habirnder Seth Singh amesema anafikiria mara
mbilimbili iwapo aendelee kuwekeza nchini au la, baada ya kuwapo kwa
tuhuma kwamba alihusika na uchotaji wa fedha katika Akaunti ya Tegeta
Escrow katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
“Nimeongelewa sana kiasi kwamba naona kama hakuna
hata amani ya kuwekeza Tanzania, nitajifikiria mara mbili mbili.
Wananchi wanaelewa vingine kabisa kuhusu suala hili kwa sababu ya
upotoshwaji,” alisema Singh alipozungumza na gazeti hili jana.
Singh ambaye alituhumiwa kujipatia asilimia 70 ya
hisa katika Kampuni ya IPTL isivyo halali, alisema hafikirii kuwekeza
zaidi nchini kwa sababu yamekuwapo maneno mengi na shutuma zisizo na
ukweli zilizoelekezwa kwake kuhusu sakata hilo.
Kauli ya bosi huyo wa IPTL imekuja wakati Taifa
likisubiri utekelezaji wa maazimio ya Bunge na akiwa mmojawapo wa watu
wanaotakiwa kuchunguzwa na vyombo vya dola ili akibainika kufanya
makosa, afikishwe mahakamani.
Jana, Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba
alimtaka Rais Jakaya Kikwete kutekeleza haraka maazimio manane
yaliyotolewa na Bunge dhidi ya ufisadi wa sakata la escrow.
“Rais hatakiwi kukaa kimya, atoe tamko la haraka
ili kuwaondoa viongozi hao. Hata Waziri Mkuu anatakiwa kuwajibishwa kwa
sababu ni chanzo cha udhaifu huo,” alisema Profesa Lipumba alipokuwa
akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa Jumuiya ya Wanawake wa CUF (JUKECUF).
Jana, Ngeleja ambaye pia ni Mbunge wa Sengerema
alisema: “Kwangu ni kama hukumu imetangulia mashtaka kwa sababu sikuwahi
kuitwa kuhojiwa mahali popote, ila ninauheshimu uamuzi wa Bunge.”
Kwa upande wake, Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed
Chande Othman alisema hayuko tayari kuzungumzia masuala ya kashfa ya
Akaunti ya Escrow pamoja na mwingiliano wa mihimili miwili, Bunge na
Mahakama kwa kuwa siyo wakati wake.
Wakati hayo yakiendelea, uongozi wa Benki ya
Stanbic Tanzania nao ulitoa taarifa ya kukana kuhusika katika
utakatishaji fedha za Akaunti ya Tegeta Escrow, baada ya Bunge kupitisha
azimio la kuitaka mamlaka husika za kifedha kuichunguza.
Malamiko ya Singh
Singh alisema kampuni yake imekuwa ikiuza umeme
kwa bei nafuu; senti nane kuliko kampuni nyingine, lakini bado
anaonekana kuwa na makosa.
“Kuuza umeme kwa senti nane kwa megawati ni bei
nafuu sana lakini mbona naonekana kama nina makosa? Ndiyo maana ninasema
nitafikiria mara mbili kuwauzia umeme,” alisema.
Kauli ya Ngeleja
Jaji Mkuu agoma
Stanbic yakana
Masele ajigamba
Alisema kampuni nyingine za kufua umeme zinauza umeme mara mbili
ya bei kuliko yake, lakini bado anaonekana si mwekezaji mzuri huku
mazuri yote aliyoyafanya nchini yakisahauliwa.
Alisema anashangazwa na kauli za wabunge na baadhi
ya wanasiasa kuwa anatakiwa kukamatwa kwa kukwepa kodi na kujipatia
fedha isivyo halali na kusema haoni kosa alilolifanya mpaka sasa.
“Wanikamate kwa lipi? Hata kutaifisha mali zangu au mitambo hawawezi kabisa hiyo ni kazi ya Mahakama,” alisema.
Alisema wanaomtuhumu kuwa kaiba fedha za umma
hawana hoja na kwamba kama ingekuwa kweli, waliotakiwa kulalamika ni
mmiliki mwenza wa zamani wa IPTL, James Rugemalira na raia wa Malaysia,
aliyemtaja kwa jina moja la Barbin... “Wenyewe wahusika hawajasema kama
wameibiwa lakini leo naambiwa na Bunge nimeiba na wanataka kutaifisha
mali zangu inashangaza sana.”
Alisema ameshangazwa na jinsi Bunge lilivyomhukumu
bila kupewa nafasi ya kujitetea... “Wao wanajadili bungeni, Mahakama
haijatoa hukumu lakini wanamhukumu mtu ambaye hayupo hapo, hawajasikia
utetezi wake. Inashangaza sana, kwa nini Mahakama isifanyie kazi suala
hili na kutoa hukumu?”
Kuhusu utata wa uraia wake, Singh alisema hakuna
ukweli wowote kuwa yeye ni Mkenya au wa Afrika Kusini na kusisitiza kuwa
ni Mtanzania, mzaliwa wa Iringa. “Mimi ni Mtanzania, unafikiri mimi
Mhindi?” alihoji Singh.
Kauli ya Ngeleja
Kwa upande wake, Ngeleja naye alilalamikia
kutohojiwa na kusema: “Siwezi kufahamu kwa nini sikuitwa kuhojiwa maana
hata maaskofu nimesikia kwenye vyombo vya habari kwamba nao wanalalamika
hawakuhojiwa, pengine inawezekana muda ulikuwa mfupi, hilo sifahamu.”
Ngeleja ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Nishati na
Madini kabla ya kung’olewa katika nafasi hiyo alisema katika mazingira
ya sasa hawezi kuzungumzia fedha zinazodaiwa kuingizwa katika akaunti
yake, hadi pale wenye mamlaka zitakapotekeleza maazimio ya Bunge.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Usajili wa
Vizazi na Vifo (Rita), Philip Saliboko alisema anasubiri uchunguzi
ufanyike ili kubaini ukweli juu ya kuhusishwa na mgawo wa Sh40.4 milioni
zilizochotwa kutoka akaunti hiyo.
“Unataka nizungumze nini sasa? Taarifa zimesomwa na kutangazwa, tusubiri huo uchunguzi unaotakiwa kufanyika,” alisema.
Jaji Mkuu agoma
Akizungumza baada ya mkutano wa viongozi wa Mahakama na vyombo
vya habari uliofanyika Dar es Salaam jana, Jaji Mkuu Chande alisema:
“Mambo hayo yameshajadiliwa na hapa tulipo si mahala pake.”
Aliombwa kutoa kauli yake kuhusu baadhi ya majaji
kuhusishwa na kashfa ya hiyo na kile kilichoelezwa kuwa kuingiliana kwa
mihimili ya Bunge na Mahakama katika kushughulikia suala hilo.
Hata hivyo, mmoja wa maofisa wa Mahakama
aliyekuwapo eneo hilo, alisema suala majaji wanaotuhumiwa linanasubiri
kuundwa kwa tume ya kijaji kama ilivyoelekezwa na Bunge.
Majaji hao waliotajwa ni Aloysius Mujulizi na
Profesa Eudes Ruhangisa ambao wanadaiwa kuhamishiwa fedha kutoka kwa
akaunti ya mmojawapo wa watuhumiwa iliyopo Benki ya Mkombozi. Hadi sasa
majaji hao hawajatoa maelezo yoyote kuhusu suala hilo.
Stanbic yakana
Benki ya Stanbic jana ilitoa taarifa kwa umma
ikisema haihusiki na sakata hilo na kwamba imekuwa ikifuata sheria na
kanuni za kifedha katika utendaji wake.
“Tunapenda kuwahakikishia wateja wetu kwamba Benki
ya Stanbic siku zote inafuata masharti yote na pamoja na sheria za
maadili zilizowekwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,”
ilisema taarifa hiyo.
Benki ya Mkombozi inayomilikiwa na Kanisa Katoliki ilishatoa taarifa ikikanusha kuhusika kutakatisha fedha chafu.
“Benki inawataarifu wateja wake na Watanzania kwa
ujumla kutoyumbishwa na tuhuma hizo ambazo hazina ukweli ndani yake na
badala yake waitumie benki yao kwa shughuli za maendeleo ya nchi yetu,”
ilisema taarifa hiyo.
Msemaji wa BoT, Lwaga Mwambane alisema tuhuma
dhidi ya benki hizo zinafanyiwa kazi na Kitengo cha Intelijensia ya
Fedha (FIU) kilichopo chini ya Wizara ya Fedha.
Masele ajigamba
Naye Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Steven
Masele amejigamba kuwa tuhuma zilizokuwa zikielekezwa kwake kuhusu
sakata hilo ni kama kumpiga chura teke na kumwongezea mwendo.
CHANZO: MWANANCHI
Akihutubia mkutano wa uzinduzi wa kampeni za Serikali za Mitaa
mjini Shinyanga juzi, Masele alisema aliokolewa kutoka kwenye mto
uliojaa mamba na kusema wabaya wake walijua tayari wamemwangamiza na
kwamba kupona kwake kumempa nguvu ya kufanya kazi kwa bidii ili kuleta
mabadiliko katika jimbo lake la Msalala.
CHANZO: MWANANCHI

No comments:
Post a Comment