Tuhuma zinazomhusisha Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, kusimamia na kubariki mchakato ulioipa zabuni kampuni ya M/S Shumoja, ya kuendesha mradi wa treni za kisasa, jijini Dar es Salaam, bila ya kufuata sheria, zimefika bungeni.Zilifikishwa bungeni jana na Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni na kusema hatua ya serikali kutangaza kuipa kampuni hiyo zabuni hiyo, ina utata.
Treni hizo zitahudumia abiria kutoka Stesheni ya Dar es Salaam mpaka Pugu kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA).
Msemaji Mkuu wa Kambi hiyo, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji), Pauline Gekul, alitoa tuhuma hizo dhidi ya Waziri Mwakyembe, wakati akiwasilisha maoni ya kambi yake bungeni jana, kuhusu Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Ubia wa Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP) wa Mwaka 2013.
Muswada huo, ambao ulipitishwa na Bunge jana, uliwasilishwa bungeni na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji), Dk. Mary Nagu.
Gekul alisema mradi huo, ambao mkataba wake wa maelewano, ulisainiwa na mmiliki wa kampuni hiyo, Robert Shumake na Mkurugenzi wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL), huku ukishuhudiwa na Waziri Mwakyembe, Oktoba 3, mwaka huu, ni moja ya miradi inayozua maswali kwa Watanzania.
“Maswali yaliyoibuka baada ya serikali kutangaza kuipa tenda (zabuni) kampuni ya Shumoja ni pamoja na lini serikali ama wakala ama shirika ama wizara yake ilitangaza tenda ya mradi wa treni kutoka Stesheni mpaka Pugu kupitia Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere?” alihoji Gekul.
Pia alisema hadi sasa haijulikani ni lini serikali ilifanya upembuzi yakinifu kuhusu mradi huo wa reli kwa kufuata taratibu kama zinavyoainishwa na Sheria ya PPP ya mwaka 2010, ambayo tunaenda kuifanyia marekebisho?
Vilevile, alisema haijulikani ni kampuni ngapi, ambazo ziliomba zabuni ya ukandarasi wa treni na kampuni hiyo ilishinda zabuni hiyo kwa vigezo gani?
”Kwa kifupi, ni kuwa Waziri Mwakyembe na wizara yake walikiuka Sheria ya PPP,” alisema Gekul.
Alivitaja vifungu vya sheria hiyo, ambavyo Waziri Mwakyembe na wizara yake walikiuka kuwa ni pamoja na kifungu cha 4 (1) na (2) kinachomtaka waziri kutangaza katika Gazeti la Serikali miradi mbalimbali inayotegemewa kufanywa na sekta ya umma kwa ubia na sekta binafsi.
Kifungu kingine ni cha 5 (1), ambacho kinaitaka mamlaka inayohusika, kufanya upembuzi yakinifu baada ya kupembua mradi, ambao utafanywa kwenye ubia.
Kingine ni cha 9 kinachotaka mzabuni kutoa nyaraka mbalimbali za miradi, ikiwamo jina, mahesabu yaliyofanyiwa ukaguzi pamoja na vielelezo vya uwezo wa kifedha, pamoja na taarifa zinazoonyesha.
Alihoji haraka iliyokuwapo ya kutekeleza mradi huo, ambao umekiuka Sheria ya PPP bila kushindana na kampuni hiyo.
Gekul alisema ingekuwa vyema kama serikali ingetoa bayana undani wa mkataba wa mradi huo, ambao Watanzania hawajawahi kusikia ukitangazwa ili kutoa fursa kwa wazabuni wenye uwezo kushindana zabuni hiyo zaidi ya kuona na kuusikia mradi siku ya utiaji wa saini.
Alisema wanajua kwamba, serikali ikishabanwa kutoa majibu juu ya uvunjwaji wa sheria, imekuwa ikija na majibu ya kejeli.
“Kambi ya Upinzani Bungeni inataka kuwaeleza Watanzania kuwa sheria zilizotungwa na Bunge zimkuwa zikipandishwa ili kupitisha miradi, ambayo baadaye inageuka kuwa mzigo kwa Watanzania kama ilivyokuwa IPTL, Escrow,” alisema Gekul.
Alisema wanaelewa kuwa kuna adha ya usafiri katika Jiji la Dar es Salaam na kwamba wamekuwa wakipigania haki ya wakazi wa jiji hilo.
“Lakini ukweli unabaki palepale kuwa Waziri wa Uchukuzi alisimamia mchakato wa mradi ambao ulikiuka sheria ambao ikiwa utashindikana katika utekelezaji na mzigo wa uvunjwaji ama usitishwaji wa mkataba basi gharama zitarudi kwa Mtanzania,” alisema Gekul.
Aliongeza: “Hoja hapa ni kweli Kamati (ya Bunge) ya Miundombinu imepitia mkataba huu wa reli za kisasa kwa ajili ya kurahisisha usafiri Dar es Salaam? Pamoja na mikataba mingine ya uwekezaji katika wizara anayoisimamia yeye?”
Alihoji ikiwa kuna usiri juu ya mikataba ya miradi inayofanywa kupitia PPP, ni kwa vipi wananchi wasizue maswali juu ya saa ya rais na utoaji wa mradi wa treni ziendazo kasi kwa mmiliki wake, ambaye anatambulika kama Balozi wa Heshima wa Tanzania nchini Marekani?
Alisema kuna azimio la Bunge lililotokana na Kamati Teule ya Bunge iliyokuwa chini ya Dk. Mwakyembe, iliyochunguza kashfa ya kampuni hewa ya Richmond, linaloshutumu utaratibu uliorithiwa na baadhi ya Watanzania kutoka kwa Wakoloni wa kuiona mikataba ya kibiashara kuwa ni siri hata kwa walipakodi wenyewe na kuwa uwanja pekee wa watendaji.
”Kwa masikitiko, waziri huyo sasa hivi anashindwa kutembea kwenye maneno yake na badala yake mikataba anataka iwe kwa fasta fasta na kuwa ni siri bila kamati za kisekta kuipitia,” alisema Gekul.
UHUSIANO WA SERIKALI, WAWEKEZAJI WA NDANI
Alisema ni jambo linalosikitisha kuwa pamoja na kuwa wawekezaji wa ndani ya nchi wanatambulika katika jumuiya za kimataifa, huku wengine wakipata sifa katika majarida makubwa duniani, baadhi ya viongozi na hasa mawaziri, wamekuwa na wakaidharau kiasi cha kutamka hadharani kuwa wanafaa kuwekeza katika matunda na juisi.
Gekul alisema jamno hilo ni la hatari katika uchumi wa Taifa kwa kuwa baadhi ya wawekezaji wa nje wameonyesha wasiwasi katika kuingia ubia na wawekezaji wa ndani kwa kuhofia uwezo wao.
”Leo tukiwa tunaleta marekebisho ya muswada huu, viongozi wa kisiasa, ambao wametoa kauli za dharau dhidi ya wawekezaji wa ndani, hawajawahi kukemewa na serikali wala kuwajibika kwa kauli zao,” alisema Gekul.
Aliongeza: “Je, ni kweli kuwa serikali ya CCM inawathamini Watanzania wenye uwezo wa kuwekeza kupitia ubia baina ya sekta ya umma na sekta binafsi?Kadri serikali inavyohangaika kuwavutia wawekezaji wa nje kwenye sekta zote hususan gesi asilia.”
“Pia ikumbuke kuwa inao wajibu wa kuwajengea wazawa mazingira ya kisera na kisheria kuwa wamiliki wa uchumi mkubwa wa taifa hili sambamba na wawekezaji hao ili kuondokana na umaskini wa kipato.”
Alisema wakati Rais Jakaya Kikwete akizunguka nchi mbalimbali duniani kutafuta wawekezaji kuingia ubia na sekta ya umma nchini, Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, amekuwa akizunguka kuwahimiza Wakenya wazawa kuwekeza katika nchi yao ili siyo tu kuinua uchumi wa Taifa lao, bali pia kunyanyua pato la taifa kutokana na uwekezaji wa ndani.
UKUZAJI WA AJIRA KWA KUPITIA PPP
Alisema tatizo lingine la kisera linalotakiwa kupatiwa ufumbuzi ni suala la wawekezaji wa kigeni kutotoa nafasi za ajira kwa wazawa ama kuwapa wazawa nafasi na fursa, ambazo hazina kipato lingani kwa wazawa, hivyo akashauri muswada huo uangalie upya ili kujumuisha changamoto za ajira zinazotokana na ubia baina ya sekta ya umma na sekta binafsi.
Gekul alisema kuna ulazima wa kuangalia mazingira ya ujumla yanayohusiana na sera na sheria nyingine zinazoshabihiana na PPP.

CHANZO: NIPASHE

No comments:
Post a Comment