Mkurugenzi wa Utafiti wa Uchumi na Sera wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Joseph Massawe (kushoto), akisalimiana na Balozi wa Japan nchini, Masaki Okada, wakati wa uzinduzi wa Kampuni ya Samurai Trading Limited, jijini Dar es Salaam wiki iliyopita.(Picha: Mpiga Picha Wetu)
Balozi wa Japan Tanzania, Masaki Okada, amesema uhusiano wa kibiashara kati ya Tanzania na Japan unazidi kuwa mzuri na kielelezo kimojawapo ni kampuni zaidi kutoka nchini kwake kufungua shughuli zake jijini Dar es Salaam.
Alisema hayo jijini Dar es Salaam wiki iliyopita wakati wa ufunguzi wa ofisi za kampuni ya Samurai Japan Trading Limited inayojihusisha na uuzaji wa magari.
“Japan ina teknolojia ya kuaminika ambayo tungependa kuieneza Tanzania kwa kuwa uhusiano wetu ni mzuri kwa muda mrefu,” alisema Okada.
Akizungumza kwenye tukio hilo, Mkurugenzi wa Utafiti wa Uchumi na Sera wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dk. Joseph Massawe, aliwataka Wajapani kuwekeza nchini kwa sababu kuna fursa nyingi za uwekezaji na uchumi unaokua.
Alisema kiuchumi nchi iko sehemu nzuri kati ya nchi za Kiafrika jambo ambalo litawasaidia kupanua biashara yao pia kwa nchi za jirani kwa kutumia bandari kubwa iliyoko nchini.
Shabaha ya Samurai Japan Trading Ltd. ni kutoa huduma kwa wanunuzi walioko Afrika, hasa, ambazo haziwezi kutolewa kupitia mtandao.
“Pale Samurai Japan Trading magari yote yana dhamana na yako tayari kutembea.
Kufuatia ahadi hizi kampuni huuza magari ambayo yamefanyiwa ukarabati, yakiwa yako tayari kutembea na huuzwa moja kwa moja kwa mteja ili kutoa huduma kwa wanunuzi walioko Afrika bila ya kutumia mtandao,” alisema Balozi Okada.

Chanzo: NIPASHE
No comments:
Post a Comment