Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli (pichani) amesema dawa ya magari yanayozidisha uzito yanapopita barabarani imepatikana na kueleza kuwa hakutakuwa na fitina.
Pia amesema serikali iko mbioni kujenga barabara sita, kuanzia Ubungo hadi Chalinze lengo ikiwa ni kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es salam.
Alisema hayo jana wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa maendeleo ya mzani wa kisasa wa Kigwaza, uliopo Mkoa wa Pwani, ulioghalimu zaidi ya Sh. bilioni 11.
Alisema asilimia 25 ya malori hapa nchini yanaharibu barabara, hivyo kutengenezwa kwa mzani huo kutakata mzizi wa fitina kati ya Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) na madereva.
“Hakutakuwapo na ubishi tena. Gari litakalozidisha uzito, tutawatandika. Dawa yao ndiyo hii. Na ninawaeleza kuwa wataipatapata ukweli,” alisema Magufuli.
Alisema mzani huo una uwezo wa kupima magari yakiwa yanatembea na unaanza kupima gari likiwa umbali wa kilomita mbili kabla halijafika katika mzani.
Magufuli alisema serikali itatengeneza mizani mingine mitatu kama hiyo lengo likiwa ni kuokoa uharibifu wa barabara unaofanywa na watu wachache. Alisema mzani huo wa kisasa utamwezesha dereva kuona uzito halisi wa gari yake na mzigo.
“Sheria namba 30 ya mwaka 1973 ya usimamizi wa magari inaeleza wazi. Lakini kuna watu viburi wanaojifanya matajiri wanawahonga wafanyakazi wa Tanroads na wanapita, sasa solution imepatikana,” alisema.
Alisema nchi ya Marekani sheria yao inaruhusu gari kubeba tani 36.2, nchi za ulaya tani 48,Tanzania tani 56, Kenya na Uganda tani 54.
Alitoa miezi mitatu kwa mkandarasi anayejenga barabara iendayo Chuo cha Afya na Tiba cha Muhimbilli (Muhas) kinachojengwa eneo la Mloganzila awe ameshakamilisha ujenzi wake.

Chanzo: NIPASHE
No comments:
Post a Comment