Social Icons

Pages

Wednesday, August 13, 2014

RAIA WA BURUNDI ANASWA NA RISASI 144

JESHI la Polisi mkoani Kigoma, linamshikilia raia wa nchi jirani ya Burundi, Kabalashaka Rajabu, kwa kosa la kukutwa na risasi 133 za silaha aina ya SMG na 11 za Heavy Machine Gun katika begi lake. Picha na Maktaba

Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi mkoani humo, Jaffar Mohamed, alisema lilitokea Agosti 9 mwaka huu, saa tatu usiku katika eneo la Mnarani, wilayani Kasulu.

Alisema siku ya tukio, askari walikuwa kwenye msako endelevu wa kupambana na majambazi ambapo walifanikiwa kumkamata Rajabu na walipopekua begi lake, walizikuta silaha hizo.

Aliongeza kuwa, mtuhumiwa alitoka na silaha hizo nchini kwao na kuingia nazo nchini kwa lengo la kuziuza kwa wateja wake anaowafahamu; hivyo uchunguzi wa kina unaendelea kuubaini mtandao huo na atafikishwa mahakamani muda wowote.

Kwa upande wake, Mkuu wa Idara ya Uhamiaji mkoani humo, Ebrosy Mwanguko, alisema changamoto ya uhamiaji haramu inachangiwa na baadhi ya wananchi wasio wazalendo kwa Taifa lao.

Alisema wananchi hao wanashirikiana na raia wa nchi nyingine kuweka rehani usalama wa taifa lao kwa siku za usoni.


Chanzo: MAJIRA

No comments: