Chama Cha Mapinduzi (CCM)
Baadhi ya wagombea wengine ni Said Rambi (ACT-Wazalendo) kura 4,398, Rajabu Bakari (Tadea) kura 607, Ndonge Said (AFP) kura 737, Rehema Kilai (Chausta) 1,314, Mapande Kassim (NCCR-Mageuzi) kura 2,156, Ramadhani Nassoro (NRA) kura 238 na Marry Daudi (UPDP) kura 81.
Hata hivyo, mgombea ubunge kwa tiketi ya CUF katika jimbo hilo,
Juma Kondo, alisema hayatambui matokeo hayo kwa madai kwamba yamefanyika
kinyume cha taratibu za uchaguzi na haukuwa wa haki.
Alidai kuwa juzi wakati kazi ya kuhesabu matokeo ya jimbo hilo
ikiendelea, Msimamizi wa Uchaguzi aliwaambia mawakala wa vyama na
wagombea ubunge kuwa kazi hiyo imesitishwa hadi pale Tume ya Taifa ya
Uchaguzi (Nec) itakapotoa tamko la mwisho kuhusu mgogoro uliopo jimboni
hapo.
Alisema wanashangaa walipofika siku inayofuata katika Shule ya
Msingi Maji Matitu ambako ndiko majumuisho ya kura za jimbo hilo
yalikuwa yakifanyika, waliyakuta matokeo yakiwa yamebandikwa pasipo
kushirikishwa.
Aliongeza kuwa wanajipanga kufuata sheria na taratibu za kukata rufaa baada ya kushauriana na mwanasheria wao. “Matokeo haya siyatambui kwa kuwa ni ya uongo. Kwanza Mkurugenzi
alikuja kubandika wakati wagombea hatupo na hakuna sehemu yoyote
niliyosaini… Siamini kama Mkurugenzi ndiye aliyebandika,” alisema Kondo.
Naye mgombea ubunge kwa chama cha NCCR-Mageuzi, Kassim Mapande,
alisema uamuzi alioutoa Mkurugenzi, ni wake peke yake kwa kuwa
hakuwashirikisha wagombea na kwamba matokeo hayo ni ya uongo.
Msimamizi wa Uchaguzi, Kagimbo aliwataka wananchi wa jimbo hilo
kuyaheshimu matokeo hayo na kukubali matokeo yaliyotolewa na Nec pasipo
kusahau kuimarisha amani.
Alisema idadi ya wapiga kura katika jimbo hilo walioandikishwa
walikuwa ni 336,468, idadi halisi ya waliopiga kura ni 183,770 na idadi
ya kura halali ni 174,982 huku kura zilizokataliwa zikiwa 8,788.
CHANZO:
NIPASHE

No comments:
Post a Comment