
Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Dk. Maua Daftari.
Wabunge wameitupia lawama Wizara ya Afya na Ustawi
wa Jamii kwa kushindwa kutekeleza utaratibu wa utoaji matibabu bure kwa
wazee, hali ambayo imesababisha wakabiliwe na hali ngumu ya maisha na
wengine kupoteza maisha wao kwa kukosa huduma za matibabu.
Mbunge wa Viti Maalum (Chadema), Raya Ibrahim Hamis, alisema licha
ya kuwapo kwa sera ya inayotoa maelekezo kwa wazee kutibiwa bure, lakini
jambo hilo limekuwa kiini macho kutokana na wazee kunyimwa matibabu.
Alisema wazee wanapokwenda katika hospitali, vituo vya afya na
zahanati kwa ajili ya kutibiwa wakishapewa vipimo wanaambiwa wakanunue
dawa katika maduka ya dawa. Naye Mbunge wa Kibaha Mjini (CCM), Silvester Koka, alisema Wazee
wametelekezwa katika matibabu kila wanapokwenda katika dirisha maalum
kwa ajili kupewa matibabu wakati mwingine wamekuwa wakinyimwa huduma
hiyo.
Koka aliitaka serikali kuiboresha Hospitali ya Tumbi kutokana na
umuhimu wake wa kupokea wagonjwa wanaopata ajali katika barabara Kuu ya
Dar es Salaam-Morogoro.
Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Dk. Maua Daftari, alisema inashangaza
kuona bajeti ya Wizara hiyo inategemea zaidi wafadhili wa mashirika
mbalimbali, hali inayotia mashaka na kuacha maswali kwamba wafadhili hao
watakapokosekana Wizara itajiendeshaje.
Dk. Daftari alisema ufike wakati serikali iongeze bajeti ya Wizara
ya Afya kutokana na umuhimu wake kama ilivyo kwa Wizara ya Ujenzi. Aidha, wabunge hao walalamikia upungufu wa vitanda katika wodi za
wazazi hali inayosababisha kulala wawili wawili katika kitanda kimoja.
CHANZO:
NIPASHE
No comments:
Post a Comment