Mahakama ya 
Hakimu Mkazi Kisutu imewaona wafanyakazi wanane wa Benki Kuu ya Tanzania
 (BoT) wanaokabiliwa na tuhuma za kughushi vyeti na kutoa hati za uongo 
wana kesi ya kujibu.
Uamuzi huo ulitolewa jana na Hakimu Mkazi, 
Nyigulile Mwaseba baada ya kupitia ushahidi uliotolewa na mashahidi 
wanane wa upande wa mashtaka pamoja na vielelezo vilivyowasilishwa 
mahakamani hapo.
                
              
Baada ya Hakimu Mwaseba kutoa uamuzi huo, alisema 
Juni 17 na 18, 2015, washtakiwa hao ambao wanadaiwa kuwa ni watoto wa 
vigogo wa Serikali wataanza kutoa ushahidi wa utetezi dhidi ya mashtaka 
yanayowakabili.
Wafanyakazi hao ni Justina Mungai, Christina 
Ntemi, Siamini Kombakono, Janeth Mahenge, Beatha Massawe, Jacquiline 
Juma, Philimina Mutagurwa na Amina Mwinchumu.
Washtakiwa hao kwa pamoja wanadaiwa kughushi vyeti vya kuhitimu kidato cha nne na kutoa hati za uongo kwa mwajiri wao, BoT.
Washtakiwa Mungai, Massawe na Mwinchumu, wanadaiwa
 kughushi vyeti hivyo mwaka 2001, wakati Ntemi, Kombakono, Mahenge na 
Mutagurwa wanadaiwa kughushi vyeti hivyo mwaka 2002.
Wanadaiwa kughushi vyeti vya kuhitimu kidato cha 
nne na kutoa BoT hati za uongo wakionyesha kuwa vimetolewa na Baraza la 
Mitihani la Taifa wakati siyo kweli. Washtakiwa hao ambao awali 
waliyakana mashtaka, wako nje kwa dhamana.
CHANZO: MWANANCHI
CHANZO: MWANANCHI

No comments:
Post a Comment