
Kiongozi Mkuu wa Chama cha Alliance for Change and
 Transparency ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, amesema kuwa vyama vingi vya 
siasa nchini,vinasumbuliwa na uroho wa madaraka pamoja na vyeo.Aliongeza kuwa vyama hivyo katika mikutano yake vimekuwa vikiacha 
kueleza matatizo yanayowakabili wananchi badala yake ni kutukana mwanzo 
mwisho.
Zitto alitoa kauli hiyo juzi wakati akizungumza na wakazi wa Mji wa
 Maswa mkoani Simiyu, katika uwanja wa Madeco, wakati wakihitimisha 
ziara yakukitambulisha chama katika mikoa 12 nchini.
Alisema uroho wa kutaka madaraka na vyeo kwa baadhi ya wanachama na
 viongozi wa vyama hivyo, limekuwa tatizo kubwa na kuvifanya kushindwa 
kupambana kutetea hali za Watanzania ambao niwengi wao ni maskini wa 
kupindukia.
“Baadhi ya vyama vya siasa hapa nchini kazi yao ni matusi tu 
katikamikutano yao pamoja na kutambiana, vinashindwa kuwaeleza 
wananchiwanavyonyonywa na rasilimali zao zinavyonufaisha wachache, 
lakini piatamaa ya madaraka pamoja vyeo katika vyama hivyo ni tatizo,” 
alisema Zitto.
CHANZO:
     NIPASHE
    

No comments:
Post a Comment