Mbunge wa Mtambile (CUF), Masoud Abdallah Salim.
Wafuasi 11 wa Chama cha Wananchi (CUF) wamevamiwa
na kujeruhiwa na watu wasiojulikana wakati wakitokea katika mkutano wa
hadhara wa chama hicho.
Tukio hilo lilitokea juzi jioni eneo la Fuoni Jitimai, wakati wakirudi nyumbani baada ya mkutano huo, uliofanyika Makunduchi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Unguja, Juma Sadi, alisema watu
wasiojulikana waliwajeruhi wafuasi hao, ambao walikuwa katika gari na
majeruhi hao kukimbizwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja na baadhi yao
wamepewa ruhusa na wengine wamelazwa.
Kamanda Sadi alisema Jeshi la Polisi linaendelea kufanya uchunguzi ili kuwatia mbaroni waliohusika. Wakati huo huo, Mbunge wa Mtambile (CUF), Masoud Abdallah Salim,
jana alilitaka Bunge lijadili kwa dharura hali ya amani visiwani
Zanzibar kwa maelezo kuwa wanachama wa CUF, wamepigwa na kujeruhiwa.
Alisema kupigwa kwa wafuasi na wanachama wa CUF kunahatarisha amani
visiwani humo na Tanzania kwa ujumla hivyo, akaliomba Bunge lijadili
hali hiyo. Akijibu mwongozo huo, Spika wa Bunge, Anne Makinda, alimtaka
aandike hoja yake na aiwasilishe kwa Katibu wa Bunge kwa njia ya
maandishi.
CHANZO:
NIPASHE
No comments:
Post a Comment