Mwanamuziki mwenye uwezo na mvuto jukwaani, Juma
Nature amesema kuwa hana mpango wa kugombea ubunge katika Jimbo la
Temeke mwaka huu, licha ya awali kutangaza nia hiyo.
Nature ametoa kauli hiyo huku wasanii wengine wakitangaza nia ya kuwania ubunge majimbo mbalimbali. Wasanii watakaowania ubunge mwaka huu ni pamoja na Mr II ambaye atatetea ubunge wake wa Mbeya Mjini, Afande Sele, Kalapina, Chopa Mchopanga, JB ambao wametangaza nia zao kupitia vyama tofauti.

Nature ambaye hajawahi kutangaza chama
anachokipigia upatu, alisema kuwa ingawa alifuatwa na watu wengi
waliomshawishi kugombea nafasi hiyo, lakini atafanya hivyo mwaka 2020.
“Ubunge Temeke, nitapita tu. Wenyewe wanajua
kwamba mimi naweza kuwasaidia. Kwa sasa nimewaachia kina Profesa Jay na
wengine wachukue nafasi hizo, ila miaka mitano injayo usishangae
ukanikuta pale mjengoni nimevaa suti nikiwakilisha wananchi. Kwa sasa
sijaamua na malengo yangu ni mwaka 2020,” alisema Nature. Alisema kuwa akipata nafasi ya kuwa mbunge, jambo
la kwanza kufanya kwa wananchi wake ni kushughulikia kero zilizopo hasa
Barabara ya Mbagala.
“Barabara ndiyo kipaumbele, kwani mvua ikinyesha
kidogo ni shida, ile hospitali ya Temeke ni ndogo, kumwona daktari ni
kazi ngumu. Pia, soko siyo safi, inatakiwa vichimbwe visima na kujengwa
vyoo kwani watu wanachafua sana mazingira. Temeke mitaro ni mibovu, mvua
ikinyesha ni maafa kwa sababu watu wamejenga kiholela,” alisema msanii
huyo. Alifafanua kuwa wakati wake ukifika atagombea
ubunge kupitia chama chochote atakachoona kina msingi mzuri. “Lakini kwa
sasa bado sijaona ni chama kipi ngangari,” alisema .
CHANZO: MWANANCHI

No comments:
Post a Comment