Vyombo vya
usalama nchini Kenya, vinawashikilia wasichana watatu akiwamo Mtanzania,
kwa kile kunachodaiwa kutaka kujiunga na kundi la kigaidi la al-Shabaab
huko Somalia.
Taarifa kutoka kwa Kamishna wa Polisi Jimbo la El -Wak, mpakani mwa Kenya na Somalia, Nelson Marwa amesema Mtanzania aliyekamatwa, alijieleza kuwa ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Afrika, Sudan. Mtanzania huyo, Ummul-Khayr Sadir Abdul (19), mwenyeji wa Zanzibar, anatajwa kuwa kiongozi wa kundi hilo lililopanga kujiunga na al-Shabaab.
Taarifa kutoka kwa Kamishna wa Polisi Jimbo la El -Wak, mpakani mwa Kenya na Somalia, Nelson Marwa amesema Mtanzania aliyekamatwa, alijieleza kuwa ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Afrika, Sudan. Mtanzania huyo, Ummul-Khayr Sadir Abdul (19), mwenyeji wa Zanzibar, anatajwa kuwa kiongozi wa kundi hilo lililopanga kujiunga na al-Shabaab.
Wasichana wengine waliokamatwa pamoja na Ummul-Khayr, ni Maryam Said Aboud na Khadija Abubakar Abdulkadir wote raia wa Kenya. “Hawa wasichana watatu, inaaminika kuwa walikuwa
wanakwenda Somalia kupata mafunzo ya kigaidi na baadaye kufanya
mashambulizi ya kujitoa mhanga,” alisema Kamishna Marwa. Akizungumzia suala hilo, Kaimu Mkurugenzi wa
Makosa ya Jinai, DCI Diwani Athumani alisema: “Tunafuatilia hatujapokea
taarifa zaidi ya hizo.”
Kamishna Marwa alisema raia hao wawili wa Kenya,
mmoja ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mount Kenya kilichopo Thika,
Jimbo Kiambu na mwingine ni mwanafunzi wa Sekondari ya Burhania, iliyopo
Malindi, Kilifi. “Serikali imepata taarifa kuhusu watu wanaokusanya
watu kutoka Afrika Mashariki ili wakajiunge na makundi ya ugaidi
nchini Somalia, wakala wetu wa usalama wamepata taarifa hizo na
kufanikisha kukamatwa kwa wasichana hao,” alisema Kamishana Marwa.
Hivi karibuni, tovuti ya al-Jazeera ilitoa taarifa
za kukamatwa kwa mkanda wa video ulioonyesha mwakilishi wa kundi la
kigaidi la Dola ya Kiislamu ya Iraq na Levant (ISIL) akimtaka kiongozi
wa kundi la al-Shabaab kuliimarisha kwa kufanya mashambulizi ya kigaidi
katika miji ya Mwanza na Dar es Salaam.
Kamishna Marwa alisema ingawa nyaraka za
wasichana hao zote zinaonyesha kuwa ni wanafunzi, lakini bado walibanwa
kwa maswali kuhusu sababu inayowapeleka nchini Somalia.
Aliongeza zaidi kuwa chanzo cha habari cha
kiusalama kilieleza kuwa nyaraka za wasichana hao zilionyesha kuwa
walikuwa wakienda kuolewa na wanajeshi wa kundi la al-Shabaab.
CHANZO: MWANANCHI
CHANZO: MWANANCHI
No comments:
Post a Comment