
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda, ametoa siku saba kwa Hospitali ya TMJ, Dar es Salaam,
kuhakikisha inajenga mtaro wa kupitisha maji machafu ili kuondokana na
majitaka hayo kuingia kwenye mitaro mipya inayojengwa.
Alisema kama hospitali hiyo itapuuza agizo hilo, ndani ya siku saba,
serikali itachukua hatua stahiki ikiwamo ya kuzuia kutoa huduma. Makonda alitoa kauli hiyo alipotembelea kwenye maeneo ya Mikocheni
kukagua miundombinu ya barabara na mitaro inayojengwa ili kudhibiti
athari za mvua zinazotarajia kunyesha wakati wowote.
Makonda, alishuhudia mtaro wa majitaka ya hospitali hiyo ukitiririsha
uchafu kuelekea kwenye mitaro mipya inayojengwa hali iliyosababisha
mitaro hiyo kujaa taka kabla ya kukamilika kwake. Mhandisi wa Manispaa ya Kinondoni, Mbaraka Mkwiya, alisema miradi ya
ujenzi wa mitaro ya maji taka kwenye bonde la mpunga unagharimu
takribani Sh. bilioni sita na barabara tano za mitaa ya Mikocheni na
Msasani ambazo zitagharimu Sh. bilioni 3.3 ambayo yote, inatarajia
kukamilika miezi michache ijayo.
CHANZO:
NIPASHE

No comments:
Post a Comment