Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiwa na meneja wa shamba, Ahmed Al Mansour.
wakati wa msafara wa kukagua na kujifunza kuhusu mradi huo wa shamba la
ng'ombe.
Ukiingia kwa gari, iwe kubwa au dogo, lazima
litamwagiwa dawa kuua wadudu ama vimelea vya magonjwa.Baada ya ukaguzi
wa gari, kinachofuata ni kufunguliwa bomba maalumu za dawa kwa ajili ya
gari iwe kubwa au dogo. Pia, kuna kijibwawa chenye maji ya dawa ili kuua
bakteria wa magonjwa kwenye matairi. Kila gari lazima litumbukie kwenye
‘kibwawa’ hicho wakati wa kuingia na kutoka.
Shamba hilo la ng’ombe wa maziwa la Al Rawabi, lipo eneo la jangwa. Sehemu kubwa ya Dubai iko jangwani, lakini imeendelezwa.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alikuwa na ziara ndefu
kutembelea nchi za Dubai na Qatar yenye lengo la kutafuta wawekezaji,
fursa za biashara pamoja na kudumisha ushirikiano kati ya Tanzania na
nchi hizo za Kiarabu. Wakati wa ziara yake, Waziri Mkuu na ujumbe wake,
alipata fursa ya kutembelea shamba hilo na kujionea shughuli mbalimbali
kuanzia utunzaji, kulisha, kukamua, uhifadhi wa maziwa, kuzalishwa
kiwandani, kufungwa hadi kumfikia mlaji.
Katika ziara hiyo aliyofuatana na mawaziri, wakuu
wa mikoa na wabunge, kati ya vitu vilivyovutia zaidi ni shamba hilo la
ng’ombe lililopo jangwani, lakini ngombe wake wote wana afya, wanakula
vizuri na hata kutoa maziwa kwa wingi.
Kwanza; aina ya ng’ombe wanaotunzwa hapo hadi uzalishaji wa maziwa. Meneja wa shamba hilo, Ahmed Al Mansour, anasema kuwa walianza na ng’ombe 500, lakini sasa wana ng’ombe 12,000.
“Shamba hili ni muungano wa wafugaji watano ambao
walikuwa na lengo moja la kuzalisha maziwa, walipeleka mapendekezo
serikalini na serikali ilikubali kusaidia kama kikundi kwa baadhi ya
maeneo,” alisema. Alisema kuwa Serikali imewapa msaada wa kutosha katika kufanikisha kazi zao.
Mifugo
Eneo la mifugo limetengwa kulingana na aina ya
ng’ombe. Kuna eneo maalumu kwa ng’ombe wanaozaliwa, eneo la ng’ombe
wanaoendelea kukua na maeneo mengine ni kwa ng’ombe waliokamilika. Ng’ombe mmoja aliyekamilika, hutoa lita 64 za maziwa. Ng’ombe wa
kawaida wa Tanzania hutoa wastani wa lita 15 hadi 20 kwa siku ikiwa ni
mara tatu ya ng’ombe hao. Ng’ombe hao huangaliwa saa 24 na madaktari wa mifugo wapatao 300 ambao hupokezana kwa zamu.
Katika eneo la kukamulia, ni mashine tu ndizo
zinazofanya kazi na mashine za kukamua zimeunganishwa na mipira maalum
ambayo huyapeleka maziwa moja kwa moja kiwandani. Eneo la shamba kuna
kiwanda cha kusindika maziwa katika ujazo mbalimbali na kupelekwa katika
masoko ya ndani na nje ya Dubai.
Kiwanda cha Al-Rawabi kilichoanzishwa miaka 25 iliyopita, ndicho kinachotoa huduma ya maziwa Dubai nzima. Al Mansour anasema ng’ombe pamoja na shamba kuwa na ng’ombe wengi, lakini wote huogeshwa na wanapolala hujisikia raha. Anasema kuwa kama shamba, walitengeneza mabomba ya majosho ya kutosha kwa ajili ya kuwaogeshea.
Al Mansour anasema pia kuwa kati ya ng’ombe 12,000
zaidi ya ng’ombe 3,000 huwa na mimba na hutoa maziwa mengi na hupatiwa
huduma maalumu na hawa huogeshwa mara tatu kwa siku na hata kabla ya
kukamuliwa. Ng’ombe wengine huogeshwa mara moja kwa siku na
pia hulishwa zaidi chakula, mashudu, mahindi na majani vijavyotengenezwa
na kiwanda kilichopo eneo hilo.
Chakula kinachotengenezwa kina mchanganyiko wa vitamini kinachosaidia wazalishe maziwa zaidi. Anasema huagiza majani kutoka Afrika Kusini, Marekani na nchi nyingine za Ulaya tani kwa tani na huwa na akiba ya muda mrefu. Katika shamba hilo, kuna kitengo cha kuhifadhia chakula hicho na mashine za kuchanganya majani hayo makavu na vitamini.
Hamad anasema kuwa mara nyingi wakati wa joto,
uzalishaji maziwa hupungua kwa asilimia 40, lakini kinachofanyika ni
kuhakikisha ng’ombe wanaishi katika mazingira mazuri kwa kujenga maeneo
yanayotengeneza ubaridi. Mabanda mengi yamefungwa feni kubwa pamoja na mabanda yenye
kutengeneza ubaridi kwa ajili ya kipindi cha joto na mpango umesaidia
kupunguza kiasi cha joto kutoka nyuzijoto 50 hadi 30. Meneja wa Kitengo cha Uzalishaji, Nasser Hassan
anasema kuwa miezi ya Juni, Julai na Agosti huwa ya joto kali na
kupunguza uzalishaji wa maziwa. Hata hivyo, anasema kuwa pamoja na changamoto
hizo, mpango uliopo ni kuongeza uzalishaji hadi kufikia lita 170,000 na
zaidi ni lita kufikia 200,000 kwa siku.
Waziri wa Mifugo
CHANZO: MWANANCHI
Kwa sasa, katika saa 21 kila siku, ng’ombe 210 wanakamuliwa ndani ya dakika saba.
Aina ya ng’ombe wanaofugwa hapo ni maalumu kwa kutoa maziwa mengi na hupatikana zaidi Uholanzi na Ujerumani. Mpango mwingine endelevu uliopo ni kufungua shamba
kama hilo, eneo la Liwa, Abu Dhabi umbali wa kilomita 120 likianza na
ng’ombe 6,000. Mashamba hayo yanalengwa katika masoko yote ya Falme za Kiarabu, Qatar na Oman ndani miaka mitano ijayo.
Waziri wa Mifugo
Akizungumzia hali hiyo, Waziri wa Maendeleo ya
Mifugo na Uvuvi, Dk Titus Kamani anasema kuwa atapeleka wataalamu wake
wa mifugo kuona jinsi gani ya kuanzisha mashamba hayo Tanzania. Akizungumza baada ya kutembelea shamba hilo, Dk
Kamani anasema kuwa Tanzania ina maeneo ya kutosha kwa ufugaji, majani
na maji ikilinganisha na Dubai ambao sehemu kubwa ni jangwa.
“Tutakwenda kuangalia muundo wa Ranchi ya Ruvu na
Kongwa kuona jinsi ya kuziendeleza kwa kufuga ng’ombe wa kisasa wa
maziwa kama ilivyo kwa Al Rawabi,” alisema. Dk Kamani alisema pia kuwa wanataka kuunganisha
wafugaji kuona jinsi gani wanaweza kufikia lengo kama ilivyo kwa shamba
la Al Rawabi.
CHANZO: MWANANCHI

No comments:
Post a Comment