Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC)
imeagiza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Mahusiano na Uratibu, Stephen
Wassira, kuondoka kwenye nyumba ya Bodi ya Sukari ama alipe kodi.
PAC imetaka Wassira anayekaa bure kwenye nyumba hiyo aandikiwe barua kupewa maagizo hayo.
Mwenyekiti wa kamati hiyo, Zitto Kabwe, alisema alipotoa maamuzi hayo
jana jijini Dar es Salaam. Aliitaka bodi hiyo kumuandikia baruakwa
vile anaitumia nyumba hiyo tangu alipokuwa Waziri wa Kilimo, Chakula na
Ushirika hadi sasa, bila malipo.Hata hivyo, ilielezwa kuwa baada ya kumaliza muda wake, Wassira aliiomba bodi hiyo imruhusu aendelee kuitumia nyumba hiyo kwa muda lakini matokeo yake hajaiachia. Wajumbe wa PAC walihoji ni kwa nini Waziri Wassira kuendelea kuitumia nyumba hiyo iliyopo Masaki kwa kipindi chote tangu mwaka 2010 hadi sasa wakati ni mali ya bodi hiyo na kwamba muda wake wa kuitumia ulikwisha.
Kabwe alimuagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika kumuandikia barua Katibu Kiongozi wa Ikulu, Balozi Ombeni Sefue, kuhusu suala hilo na kama wanataka kuitumia nyumba hiyo walipe kodi na malimbikizo kuanzia mwaka 2010. Wajumbe hao walitaka kupatiwa nakala ya barua hiyo keshokutwa na kwamba hati ya nyumba isibadilishwe ibakie kuwa ni mali ya bodi hiyo.
CHANZO:
NIPASHE
No comments:
Post a Comment