Tofauti na miaka mitano iliyopita, mwaka huu ulimwengu umeshuhudia uvumbuzi
wa hali ya juu katika utengenezaji wa simu za kisasa. Jambo zuri ni kuwa
matoleo karibu yote ya simu hizo yalifanikiwa kuzinduliwa hapa nchini mwezi
mmoja au miezi michache tu baada ya kutengenezwa na kampuni husika.
Baadhi ya
Watanzania nao wamekuwa wakizichangamkia na kujumuika na ulimwengu wa
teknolojia hiyo ya hali ya juu. Zifuatazo ni miongoni mwa matoleo ya simu ambayo yamebaki gumzo ulimwenguni
mpaka sasa.
Huawei Ascend Mate 7
Simu hii ilikuja na teknolojia ya
king’amuzi cha alama za vidole kuongeza usalama wa taarifa za mtumiaji. Simu
hii inayotumia mtandao wa 4G, imekuja ikiwa katika matoleo mawili ya
laini moja na mbili. Kioo chake kilichotengenezwa kwa madini ya Sapphire kina
ukubwa wa nchi 6 huku uwezo wa ndani wa kuhifadhi taarifa ukiwa ni 64GB na Ram
ya 3GB. Toleo hilo huenda likawa la mwisho kuzinduliwa kwa kuwa zimesalia wiki
mbili mwaka uishe na hadi sasa hakuna fununu za kampuni nyingine kuzindua simu
yake mpya hapa nchini.
LG G3
Baada ya kutamba sokoni na G2, kampuni ya LG ilitoa toleo la G3 ambalo ndilo
liliobaki kinara ndani kampuni hiyo hadi sasa. Watanzania wanaokwenda na wakati
walianza kuzipata simu hizo sokoni kuanzia mwezi Septemba mwaka huu. G3 huenda
ndiyo mshindani mkuu wa S5 kwa mwaka huu na ina kioo chenye ukubwa wa nchi 5.9.
Pamoja na sifa hizo simu imeokosolewa kwa kuwa na sauti dhaifu na nyembamba
ambayo baadhi wameonekana kutovutiwa nayo. Utendaji wa betri unaoenekana kuwa
wa kawaida na huisha haraka pale kioo chake QHD kinapoongezwa mwanga wa juu. Hata
hivyo, Meneja Mkuu wa kitengo cha simu za LG Afrika Mashariki, Hyon Kim,
anaeleza kuwa wameongeza ufanisi wa betri hizo hadi uwezo wa 3000mAh ambapo
chaji inadumu kwa muda mrefu.
iPhone 6 na iPhone 6 plus
Kwa mwaka huu katika nyanja za usanifu, Apple walitia fora. Hiyo ndiyo lugha
rahisi unayoweza kuelezea uvumbuzi ambao kampuni imeuendeleza hata baada ya
kutofanikiwa kwa kiasi kikubwa katika iPhone 5c na iPhone 5s mwaka jana. Matoleo
mapya ya iPhone 6 na iPhone 6 plus yanakaribiana kwa kiwango kikubwa na
kutofautiana vitu vichache, ila iPhone 6 plus ni bora zaidi kwa ukubwa wa kioo
cha nchi 5.5 dhidi ya 4.7. Hata hivyo, siku kadhaa baada ya kuanza kuuzwa
zilizuka taarifa za iPhone 6 plus kujipinda ikiweka kidogo mfukoni na kukaa
kiasi cha kuwashtua wengi waliokuwa wamezinunua au waliokuwa na mpango wa
kuzinunua. Wataalamu mbalimbali walionyesha kupitia vyombo vya habari vya
kimataifa namna simu hiyo ilivyokuwa ikijikunja kidogo kutokana na wa
kasha lake la bati kuwa laini.
Samsung Galaxy S5
Ubunifu wa hali ya juu. Hilo neno uanaloweza kuzungumza katika uvumbuzi
ulifanyika katika simu hii dada wa Galaxy S5. Ni simu ya wenye fedha na
wanaotaka kurahisha kazi zao kupitia viganja. Simu hii iliongezwa ulinzi kwa
kuwekewa king’amuzi cha ulinzi na programu lukuki za kiafya na kikazi. kiwango
kikubwa na kutofautiana vitu vichache, ila iPhone 6 plus ni bora zaidi kwa
ukubwa wa kioo cha nchi 5.5 dhidi ya 4.7. Hata hivyo, siku kadhaa baada ya
kuanza kuuzwa zilizuka taarifa za iPhone 6 plus kujipinda ikiweka kidogo
mfukoni na kukaa kiasi cha kuwashtua wengi waliokuwa wamezinunua au waliokuwa
na mpango wa kuzinunua. Wataalamu mbalimbali walionyesha kupitia vyombo vya
habari vya kimataifa namna simu hiyo ilivyokuwa ikijikunja kidogo kutokana
na wa kasha lake la bati kuwa laini. Katika mitandao mbalimbali ya
kutathmini simu kama TechRadar, S5 imepata nyota 4.5 hususan katika suala la
utendaji, matumizi na thamani yake. Moja ya sifa kuu iliyoibeba simu hii ni
kasi ya kuchakata taarifa, ukubwa na uangavu wa kioo, betri na programu rafiki
kwa matumizi ya kila siku. Tovuti maarufu ya kupitia vifaa vya simu ya
technobezz lilibaini kuwa pamoja na ubora wa Samsung wengi hawakutarajia kama
ingeendelea kutoa makasha ya plastiki na pia usomaji wake wa alama za vidole
kwamba ungesumbua kutokana programu inayoendesha kuwa dhaifu.
Sony Experia E3
Sony haikutaka mwaka upite bila matoleo kadhaa na Septemba ilizundua simu
aina ya Experia E3 ambayo ndiyo kinara wake kwa sasa. E3 yenye kioo cha nchi
4.5 na kamera yenye megapixel 5 imeongezwa ubora na inajumuisha asilimia kubwa
ya huduma zilizokuwa kwenye mfululizo wa Z. Sony imeiita simu hiyo kuwa toleo
la vijana kutokana na usanifu wake ulioifanya ionekane vizuri. Hata hivyo, E3
ubora wa betri upo chini kidogo ukifananisha na Samsung Galaxy 5.
CHANZO: MWANANCHI

No comments:
Post a Comment