Social Icons

Pages

Thursday, December 04, 2014

RIPOTI: RUSHWA YATISHIA UKUAJI WA UCHUMI

Hali mbaya ya miundo mbinu ya shule, kutapakaa kwa dawa bandia na matokeo ya  uchaguzi kuamriwa kwa nguvu ya fedha, ni baadhi ya mambo yaliyoanishwa kama matokeo ya rushwa katika  sekta za umma.
Hayo ni kwa mujibu wa Ripoti ya Matokeo ya Mtizamo wa Rushwa kwa Mwaka 2014 iliyotolewa na Transparency International jana.
Ripoti hiyo imesema rushwa na mikataba ya gizani haziibi tu rasilimali kutoka kwa watu maskini walio katika mazingira magumu zaidi, bali zinahujumu pia haki na maendeleo ya uchumi, na kuharibu uaminifu wa umma kwa serikali na viongozi wake.
Ripoti hiyo inayojikita kwenye maoni ya kitaalamu toka pande zote za dunia, inaonyesha viwango vya rushwa katika sekta ya umma duniani kote na namna hali ilivyo mbaya. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, hakuna nchi ambayo imepata maksi zote, na zaidi  ya theluthi mbili ya nchi zote duniani zikipata maksi chini ya 50 kwenye kipimo kinachoanzia maksi 0.
Hiyo inamaanisha kwamba nchizote zilizo chini ya maksi 50 ndizo zinazoongoza zaidi kwa rushwa, huku zenye maksi zaidi ya 50 na kuendelea  zikionyesha kuwa zina kiasi kidogo cha rushwa.
Ripoti imesema pamoja na kuwa rushwa ni tatizo kwa nchi zote, lakini nchi inayopata maksi za chini zaidi inatoa ishara kuwa rushwa katika nchi hiyo imetapakaa sana.
Ripoti inasema hali hiyo inaonyesha pia kuwa kuna udhaifu wa kuwaadhibu wanaojihusisha na rushwa pamoja na kuwepo taasisi za umma za kupambana na rushwa zisizojali matakwa ya raia wake.

Ripoti inazitaka nchi ambazo hazina rushwa kubwa kuchukkua hatua.
Aidha inazitaka vituo vya kifedha vya Jumuiya ya Ulaya na Marekani kuungana na nchi zinazokuja juu kiuchumi, kuizuia rushwa na kuwashughulikia wanaojihusisha nayo.
Inaziasa nchi zilizo na uchumi mkubwa ulimwenguni (G20) kuchukua jukumu lao la kiungozi, na kuzuia shughuli ya utakatishaji wa fedha na pia kampuni za siri kuficha rushwa.
“Nchi zilizo za mwisho kwa rushwa, kwa maana ya kuwa na rushwa kubwa zinahitaji kuanzisha hatua madhubuti za kupamabana na rushwa kwa faida ya watu wao, na zile zisizo na rushwa kubwa zinatakiwa kuhakikisha kuwa hazisafirishi matendo ya rushwa nje ya mipaka yao,” anasema Jose Ugoz Mwenyekiti wa Transparency Interntional
Mpangilio ulivyo katika chati hiyo unaonyesha kuwa, Denmark ni nchi ya kwanza ulimwenguni ambayo imeweza kupambana na rushwa, baada kupata asilimia 92, ikifuatiwa na New Zealand asilimia 91, kisha, Finland (89), Sweden (87) na Norway (86).
Kwa upande wa Afrika nchi tano zilizopata maksi za juu ingawaje zote ziko chini ya maksi 50, ni Lesotho asilimia 49 na ni ya 55 duniani, Namibia (49) na ni ya 55 kiulimwengu, Rwanda (49) nayo ya 55, Ghana (48) na ya 61 kiulimwengu na Afrika Kusini (44) ambayo ni ya 67 duniani.
Tanzania imepata asilimia 31 na ni ya 119 kiulimwengu, ikiitangulia Uganda iliyopata asilimia 26 na ni ya 142 duniani na Kenya iliyopata asilimia 25 na ambayo ni ya 145 duniani.
 
CHANZO: NIPASHE

No comments: