Social Icons

Pages

Thursday, December 18, 2014

POLISI WAWAZUIA WALIOPITIA JKT KUANDAMANA DAR

Baadhi ya askari wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) waliokosa ajira, wakimsikiliza ofisa wa polisi aliyewataka waondoke eneo la Ocean Road jijini Dar es Salaam baada ya kufanya maandamano ya amani kutoka Jangwani kuelekea Ikulu kwa lengo la kuiomba serikali iwapatie ajira ya kudumu.
Jeshi la Polisi  Kanda Maalumu jijini Dar es Salaam limezuia  maandamano ya vijana waliopitia mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na kuwataka Kuteua viongozi watano kwenda Ikulu kwa Rais Jakaya Kikwete kuwakilisha malalamiko yao. Vijana hao ni waliopitia operesheni Mkapa, Utandawazi, Jiajili, Miaka 40, Kasi mpya, Maisha bora, Uadilifu pamoja na Kilimo kwanza toka mwaka 2000 hadi 2014.
Vijana hao  zaidi ya 300 walianza  maandamano hayo saa mbili asubuhi kutoka Jangwani  kuelekea Ikulu wakiwa wamebeba bendera zenye rangi nyekundu na vyeti walivyohitima mafunzo yao na walipofika eneo la Hospitali ya Ocean Road, polisi walizuia maandamano hayo na kuwataka kuchagua viongozi watakao wawakilisha.
Askari hao  waliwataka wengine  kuondoka eneo hilo na kutafuta eneo lenye usalama kwenda kuwasubiri viongozi wao watakapotoka Ikulu na kuwaletea majibu. Mmoja wa kiongozi wa mafunzo, Magesa Maijo, alisema lengo la maandamano yao ni kupeleka kilio  chao  kwa Rais  kutokana na kutopewa majibu sahihi kwa wizara husika.
 
CHANZO: NIPASHE

No comments: