Mto wa kuchegama watumika kuondoa uhai wa watoto wadogo ndugu wawili.
Mtanzania
aishiye Melbourne, Australia, Charles Mihayo mwenye umri wa miaka
36, aliyekuwa akituhumiwa kwa mauaji ya binti zake wawili amehukumiwa
kifungo cha maisha jela.
Mihayo ametiwa hatiani baada ya mahakama
kujiridhisha kwa ushahidi uliothibitisha kwamba aliwaua binti zake, Indiana aliyekuwa na umri wa miaka mitatu na Savannah aliyekuwa na
umri wa miaka minne kwa kuwaua kwa kuwabana kwa mito ya kulalia na hivyo
kukosa hewa. Waendesha mashtaka walisema kwamba, Mihayo alitenda
kosa hilo baada ya kuingia kwenye mgogoro mzito na mama wa watoto
aliyewahi kuwa mkewe kwa minajili ya kujilipiza kisasi. Akitoa
hukumu hiyo jaji wa mahakama kuu ya Victorian, Lex Lasry alisema ugomvi
na mkewe haikuwa sababu ya kujiaminisha kutenda kosa la mauaji na
kushangazwa na namna mtuhumiwa alivyotumia nafasi ya ugomvi na mkewe wa
zamani kuwaua watoto ili kupunguza machungu yake. Inaelezwa kuwa
Mihayo alituma ujumbe mfupi wa maneno kwa mtalaka wake kumfahamisha kuwa
ameshinda na anakubali kupoteza haki yake ya kuwaona watoto hao, kisha
akawapiga picha watoto hao wakicheza muziki muda mfupi kabla na kuwaweka
pamoja na kuwabana pumzi kwa kutumia mito ya kulalia,kisha kupiga simu
polisi na walipowasili eneo la tukio, aliwaambia "nimekamilisha,nimewaua
watoto wInaelezwa kuwa Mihayo alituma ujumbe mfupi wa maneno kwa
mtalaka wake kumfahamisha kuwa ameshinda na anakubali kupoteza haki yake
ya kuwaona watoto hao, kisha akawapiga picha watoto hao wakicheza
muziki muda mfupi kabla na kuwaweka pamoja na kuwabana pumzi kwa kutumia
mito ya kulalia,kisha kupiga simu polisi na walipowasili eneo la tukio,
aliwaambia "nimekamilisha,nimewaua watoto wangu"
CHANZO: BBC SWAHILI

No comments:
Post a Comment