Aliyekuwa
mnenguaji mahiri wa bendi ya Twanga Pepeta na Extra Bongo, Aisha Madinda
amefariki dunia leo katika Hospitali ya Mwananyamala, jiji Dar es
Salaam.
Taarifa zilizotufikia kutoka kwa watu wa karibu wa
Aisha zinasema kuwa mnenguaji huyo alifika hospitalini hapo kwa ajili
ya matibabu na mauti kumkuta hapo hapo hospitalini huku sababu za kifo
chake zikiwa bado hazijafahamika.
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mwananyamala, Dk.
Sophinias Ngonyani alithibitisha kifo hicho na kuongeza kuwa wauguzi
waliuona mwili wa marehemu ukiwa hospitalini hapo na kutoa taarifa
ambapo ulichukuliwa na kuhifadhiwa kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi.
“Hatujafahamu amekufa kwa ugonjwa gani kwasababu
hadi mauti yanamkuta alikuwa bado hajapokelewa na kupatiwa huduma, Aisha
pamoja na huyo rafiki yake wamekuwa wakihudhuria hospitalini hapa mara
kwa mara kwa ajili ya matibabu maalum,” alisema Dk Ngonyani.
Aisha anatajwa kuwa miongoni mwa wasanii wanaopata matibabu ya kuondoa Uraibu wa matumizi ya dawa za kulevya.
CHANZO: MWANANCHI

No comments:
Post a Comment