Social Icons

Pages

Tuesday, December 16, 2014

MITANDAO YA KIJAMII NA CHANGAMOTO KWA USALAMA WA TAIFA - 1

Mfano wa mitandao hii ni kama blogu, chaneli za youtube, facebook, twitter na nyingine nyingi . Mtu anaweza kutembelea mitandao ya kijamii kwa kutumia simu ya mkononi,, kompyuta na hata vifaa vingine vya mawasiliano.
Mitandao ya kijamii ni programu inayotumia Intaneti kuwezesha watu mbalimbali kuwasiliana,  kushiriki mijadala na kuweka taarifa au kubadilishana vitu mbalimbali .
Mfano wa mitandao hii ni kama blogu, chaneli za youtube, facebook, twitter na nyingine nyingi . Mtu anaweza kutembelea mitandao ya kijamii kwa kutumia simu ya mkononi,, kompyuta na hata vifaa vingine vya mawasiliano.
Tafiti mbalimbali zinaonyesha watumiaji wengi wa mitandao ya kijamii ni watu walio pweke (single), hivyo wanatumia mitandao ya kijamii kuwasiliana, kujielezea maisha yao kwa watu na kuendeleza mambo yao binafsi . Wanaweza kujitosheleza kwa kila kitu kwa kutumia mitandao ya kijamii isipokuwa kwa vitu vichache kama kula, kulala, kunywa na vinginevyo.
Kutokana na upweke huu, mtu  hatumii mitandao kwa mambo binafsi tu, lakini pia kwa makundi ambayo yeye yumo. Kwa hivyo,  mtu huyu anaweza kutumia mitandao ya kijamii kwa
maslahi ya kundi na wanachama wa kundi fulani kama vile la uhalifu.
Pia makundi pinzani yanatumia mitandao ya kijamii kuunganisha wanachama wao na kutumia dhidi ya mahasimu wao kama ni vyama vya kisiasa, biashara zenye ushindani mkubwa, wanamuziki, makundi ya kigaidi. Mitandao ya kijamii imewezesha haya yote na jinsi huduma zinavyozidi kupatikana kwa urahisi na vifaa kupungua bei,  watu wanazidi kujiunga zaidi kwenye mitandao, huku  wengine wakiendelea kupanua zaidi makundi yao.
Utafiti mwingine ulionyesha jinsi jamii inavyozidi kupata vyombo vya mawasiliano, ndivyo jamii hiyo inavyozidi kuwa kwenye uwezekano mkubwa zaidi wa kupata madhara ya kihalifu au mwingine unaohusisha matumizi ya vyombo vya mawasiliano hasa mitandao ya kijamii .
Tishio la kiusalama kutokana na utumiaji wa mitandao ya kijamii, linaanzia hapa ambapo watu wengi zaidi wanajiunga kwenye mitandao hii kwa nia mbalimbali na hapa ndipo kila nchi hasa Tanzania inatakiwa kuangalia maslahi yake kiusalama. Mitandao ya kijamii imekuwa ikitumika  na makundi ya kigaidi kwa shuguli mbalimbali kama kubadilisha watu mitazamo, kupata wanachama wapya.
Kuwasiliana na kutoa mafunzo, makundi haya yamekuwa yakitumia zaidi mitandao hii kuwasiliana na makundi mengine ya kuhalifu kwa ajili ya kukusanya michango kutokana na shughuli haramu.
Uhusiano kati ya makundi ya kigaidi na mengine ya kihalifu, umekuwa mkubwa katika mitandao ya kijamii. Uhusiano huu unawezesha makundi ya kigaidi kupata mbinu na njia nyingi za kufanya shughuli zao.
Pia wanatumia mitandao ya kijamii kusambaza propaganda na upotoshaji mwingine mwingi kuhusu shughuli za kigaidi na kufanya jamii ishtuke au kuwa na woga dhidi ya taasisi nyingine kama vyombo vya habari .
Athari ya woga huu inaweza kuwa wawekezaji kuamua kutoa mitaji yao kwenye masoko ya hisa, watu kuacha kufanya kazi na shughuli zingine za kiuchumi na kukimbia kutoka eneo moja kwenda jingine.
Inahofiwa pia makundi ya kihalifu hasa yale ya kigaidi,  yanaweza kutumia mitandao ya kijamii kusambaza habari za uwongo kuhusu matukio kama ya tetemeko la ardhi, mafuriko, mlipuko wa magonjwa ili kuchelewesha uokoaji na kusababisha madhara zaidi kwa jamii ili hatimaye wapate ushindi.

CHANZO: MWANANCHI

No comments: