Jaji Mkuu, Chade Othman akimsikiliza Rais wa Baraza la Habari Tanzania
(MCT), Jaji Thomas Mihayo (kushoto) baada ya kufungua mkutano wa wa
majaji na wahariri wa vyombo habari Dar es Salaam jana. Wa pili kushoto
ni Jaji wa Mahakama ya Biashara, Robert Makaramba na Katibu Mtendaji wa
MCT, Kajubi Mukajanga.
Jaji Mkuu Chande
Othman ametaka mahakama ziruhusu waandishi wa habari kupata taarifa za
yanayoendelea mahakamani ili kupata taarifa sahihi.
“Umefika wakati Mahakama kuondoa sababu zisizo za
msingi za kuzuia wanahabari kupata taarifa za mambo yanayoendelea
mahakamani,” alisema Jaji Othman wakati wa mkutano wa majaji na wahariri
wakuu uliofanyika jana jijini Dar es Salaam.
Hata hivyo, alionya kuwa “wanahabari wanapaswa
kuwasiliana na mahakama ili kuipa nafasi ya kujitetea pale inapoingizwa
katika tuhuma.”
Alisema mkutano huo ni sehemu muhimu ya kumaliza
matatizo ambayo yamekuwa chanzo cha malalamiko dhidi ya vyombo vya
habari, kutokana na mahakama kujifungia katika chumba na kutotoa taarifa
sahihi kwa wakati pale zinapohitajika.
Alisema wanahabari wanatakiwa kuandika ukweli kwa kufuata maadili yao na waipe mahakama nafasi ya kujitetea.
Alisema kusiwe na ugumu katika utendaji wa
mahakama na wanahabari ili kila mtu afanye kazi kwa uhakika na kuheshimu
uhuru, maadili na haki ya demokrasia ya kupata habari inayotolewa na
Katiba.
Alisema vyombo vya habari na mahakama ni nyenzo
muhimu katika kukuza utawala wa sheria na demokrasia, hivyo ushirikiano
baina ya mihimili hiyo unahitaji mtazamo mpya.
Alisema mihimili hiyo ni kimbilio la wananchi
katika kipindi hiki ambacho demokrasia ya kweli ‘inakata mizizi’ yake,
hivyo kuhitaji ushirikiano wa kipekee. Mwenyekiti wa Baraza la Habari
(MCT), Jaji Joseph Mihayo alisema Mahakama itende haki ili kurahisisha
upatikanaji wa habari.
kwa kutoa fursa kwa wananchi kupata taarifa sahihi kwa wakati kuhusu kile kinachojiri mahakamani.
CHANZO: MWANANCHI
CHANZO: MWANANCHI

No comments:
Post a Comment