Rais wa Sierra Leone Ernest Bai Koroma ametaka
kufanyika kwa msako wa nyumba hadi nyumba kwa waathiriwa wa ugonjwa wa
ebola nchini humo.
Rais
Ernest Bai Koroma wa Sierra Leone amesema kuwa msako wa nyumba kwa
nyumba unaanza kote nchini humo kuwatambua watu walio na ugonjwa hatari
wa ebola. Aidha, Rais huyo amepiga marufuku biashara siku ya Jumapili. Katika hotuba kupitia televisheni ya taifa, Koroma amesema kwamba usafiri kutoka wilaya moja hadi nyingine ni marufuku. Juma
moja lililopita, wakuu walifutilia mbali mikutano yote na sherehe za
siku kuu ya krismasi na mwaka mpya kama njia ya kukabiliana na kusambaa
zaidi kwa ebola.
Kwa mujibu wa takwimu za hivi punde kutoka
shirika la afya Duniani WHO, Sierra Leone ni taifa ambalo limeathirika
pakubwa na ebola ambapo zaidi ya visa elfu nane vimeripotiwa.
''Musiwafiche wagonjwa'',alisema rais. Mbali
na kufutilia mbali biashara za siku ya jumapili,mikakati hiyo mipya
itashirikisha mda wa kununua bidhaa siku ya jumamosi na katikati ya
wiki.
Mji wa Freetown umerekodi zaidi ya asilimia 50 ya maambukizi
ya ugonjwa wa ebola nchini Sierra leone katika kipindi cha majuma
mawili yaliopita. Mwandishi wa BBC nchini Sierra Leone Umaru Fafana amesema kuwa mikakati hiyo inalenga kudhibiti makundi ya watu. Amesema
kuwa wakaazi wa mji wa Freetown wanaendelea kujumuika katika barabara
mbali na kufanya mazoezi kwa pamoja licha ya tishio hilo la Ebola
CHANZO: BBC SWAHILI

No comments:
Post a Comment