Social Icons

Pages

Saturday, December 20, 2014

DK. MENGI AWATAKA WAANDISHI KUANDIKA HABARI ZA KUIJENGA NCHI

Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Dkt. Reginald Mengi, akiwa na wafanyakazi wa kampuni ya Hali Halisi, wakati wa uzinduzi wa tovuti ya kampuni hiyo ijulikanayo kama www.mwanahalisionline.com, jijini Dar es Salaam jana. Nyuma ya Dkt. Mengi ni Mwenyekiti wa jukwaa la wahariri, Absalom Kibanda, na watatu kulia ni Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Saed Kubenea.
Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa vyombo vya Habari nchini (Moat), Dk. Reginald Mengi, amewataka waandishi kuvua koti la woga na kuandika taarifa zenye kujenga agenda ya muelekeo wa nchi.
Akizungumza wakati akizindua gazeti la Mwanahalisi online, jijini Dar es Salaam jana, Dk. Mengi, ambaye Mwenyekiti mtendaji wa IPP, alisema wananchi wanatatizo la kujua wapi nchi yao inaelekea, hivyo kuna umuhimu wa kuhabarisha kwa kuibua vitendo viovu na ufisadi. Hata hivyo, alitahadharisha lazima taarifa hizo ziwe za kweli, zisizoegemea upande mmoja na zenye kujenga nchi na si kinyume na hapo.
“Wote tunafahamu kazi ya vyombo vya habari ku kuhabarisha, kuelimisha na kuburudisha, lakini kuna kazi nyingine ya nne nayo ni kujenga agenda kwa wananchi juu ya muelekeo wan nchi yao, tuwaambie jamii wapi  inapokwenda na mambo mbalimbali tunayokabiliana nayo kwa sasa,” alisema Dk. Mengi.  Alisema kamwe waandishi wa habari wasinyamaze kimya au kupendelea wanapoana kuna vitendo viovu vinavyofanywa na ya kupewa sifa viongozi,  badala yake waweke wazi ili kukwepa kuhusishwa na dhambi hiyo.
“Mwandishi anapokuwa kimya katika suala la uovu, naye atakuwa amefanya vibaya. kwani atakuwa ameingia katika uovu huo,”aliongeza kusema. Alimpongeza Mkurugenzi wa Kampuni ya Mwanahalisi, Sayed Kubenea, kwa kuanzisha gazeti hilo na kumtaka kuendeleza juhudi zake za kuandika habari zenye lengo la kulinda nchi bila ya kujali misukosuko anayokabiliana nayo. Akizungumzia gazeti hilo, Kubenea, alisema wananchi watalisoma bure kupitia mitandao mbalimbali na litakuwa na habari zote muhimu za uchunguzi, kijamii, biashara na michezo.
Alisema kwa kutumia mfumo huo mpya, Mwanahalisi online, litapatikana kila Jumatano na baada ya muda litatoka siku mbili kwa wiki. “Tunawashukuru wananchi kwa uvumilivu wao baada ya gazeti la Mwanahalisi kufungiwa kwa muda usiojulikana, kwa kuona chombo hiki ni mali ya uma tumeamua kuwaletea katika mtindo wa mtandao ili waweze kunufaika,” alisema Kubenea.
Kwa upande wa Katibu mtendaji wa baraza la habari nchini (MCT) Kajubi Mukajanga, alisema anaamini kuanzishwa kwa gazeti hilo itakwenda sambamba na uendelezaji wa tabia yao iliyozoeleka ya uadilifu, ushupavu, kujitoa na kutokatishwa tamaa. Alisema kutokana na mambo hayo,walifanikiwa kuibua mambo mbalimbali mabaya na kuwafanya  wananchi walipende.
CHANZO: NIPASHE

No comments: